Breaking News, Kiongozi CUF apanda mgomba barabarani

Kiongozi wa chama cha wananchi CUF wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma Bw. Vedasto Pesambili amepanda mgomba katika moja ya mashimo yaliyochimbika kwenye moja ya barabara za mjini Kibondo. 

 Kwa mujibu wa maelezo yake aliyochapisha katika ukurasa wake wa Face Book, Bw. Pesa mbili amefanya kituko hicho kama sehemu ya kumkumbusha meneja wa TARURA wilayani Kibondo kufanya matengenezo ya barabara hiyo 

 "Namshukuru meneja wa Tarura kunipa eneo la kupanda migomba, nimekuta ameshachimba mashimo, mimi kazi yangu ilikuwa kutafuta mbengu tu" ameandika Bw. Pesambili 

Pesambili ambaye huchukuliwa kama kiongozi wa kisiasa mwenye utani na mizaha kupitia mitandao ya kijamii amekuwa akikikosoa chama cha mapinduzi kwa kutumia ukurasa wake wa FB pamoja na kufanya utani na wana CCM 

Kila kukicha mwanasiasa huyu anajizolea umaarufu kwa namna anavyofuatilia mapungufu ya serikali na kuyapeperusha mitandaoni 

 Licha ya kwamba anatumia mbinu zanutani wa jadi baina ya CCM na vyama shindani Vedasto Pesambili anajigamba kuwa mtetezi wa wanuonge wolayani humo.

Post a Comment

0 Comments