Mbunge Bukoba awashika mkono shule Iliyoungua



Mbunge wa Jimbo Bukoba Mjini na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Wakili Stephano Byabato ametoa msaada wa shilingi Milioni Moja kwa ajili ya wnafunzi waliyopatwa na ajali ya moto katika shule ya Sekondary Omumwani iliyopo Bukoba Kagera.


Akikabidhi Msaada huo Mkuu wa Wilaya Bukoba Mh.Erasto Sima, amesema kuwa Mbunge Byabato ametoa kiasi hicho cha milioni moja kusaidia yale mapungufu ya mahitaji yawanafunzi waliyokumbwa na ajali hiyo ya moto iliyotokea usiku wa kuamkia tarehe 22.10.2023 na kuteketeza bweni la wanafunzi wakike wa shule hiyo.


 Aidha mkuu wa wilaya Mh.Sima amesema serikali itaendelea kufuatilia kila hatua misaada inayoletwa na wadau mbali mbali kwenye shule kama inaratibiwa kwa ufanisi mzuri.

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Musa Sima na viongozi wengine wakitembelea na kukagua athari za moto katika Bweni la Omumwani Sekondari 

Geraldina Mshema Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT)Manispaa ya bukoba nimiongoni mwa wadau waliyojitokeza kutoa msaada amewaomba wanafunzi kusitahimili hali iliyopo kwa sasa kwenye shule hiyo ili waweze kutimiza ndoto zao.


Jems M.Nyamanza mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM)Manispaa ya Bukoba amesema miundombinu ya shule kwa sasa siyo mizuri ila walimu na wanafunzi wazidi kuwa wavumilivu na watulivu maana serikali inaendelea kufanyia kazi jlchangamoto hiyo.

Sehemu ya mabaki ya vifaa vya wanafunzi vilivyoteketezwa na moto


Sambamba na hayo Laiteness Urio mwanafunzi kiongozi wa serikali ya shule hiyo amewapongeza wadau mbali mbali serikali,na zikiwemo shule mbali mbali kwa misaad waayozidi kuwapatia na kusema kuwa wao kama wanafunzi wa shule hiyo wanazidi kufarijika nakuongeza juhudi za upambanaji kwenye masomo yao na wanahaidi kuzidi kufanya vizuri licha ya changamoto hiyo ya moto kuunguza Mali zao na bweni la shule.

Imeandikwa na. Ananias Khalula, Bukoba

Post a Comment

0 Comments