Mto Malagarasi unaoingiza maji ziwa Tanganyika uko hatarini kutoweka


Na. Kadislaus Ezekiel, Buha News

Mto Malagarasi ambao ni miongoni mwa mito mikubwa katika mikoa ya magharibi ambao pia maji yake huchangia katika ustawi wa Ziwa Tanganyika na mito ya Rukuga na Congo nchini DRC uko hatarini kutoweka kutokana na mazingira yake kuharibiwa na binadamu pamoja na mifugo

Shughuli za kilimo na ufugaji zinazofanywa na wavamizi katika maeneo ya hifadhi na kingo za mto Maragalasi, zimepelekea athali kubwa za kupungua kina cha mto huo, na kuathili uwepo wa viumbe waishio majini hasa viboko na mamba.

Buha News imetembelea wilaya ya Uvinza na kasulu mkoani Kigoma na kushuhudia sehemu kubwa ya ardhi, misitu na kingo za mto huo maarufu zikiwa zimeharibiwa vipaya na kupoteza uoto wa asili katika sehemu kubwa

Katika mahojiano na Buha news, wakati wa kikao cha wadau wa uhifadhi vyanzo vya mito wilayani uvinza, Afisa maendeleo ya jamii bodi ya maji bonde la ziwa Tanganyika Bonna Mremi amesema licha ya kuweka alama za mipaka katika bonde la mto huo bado uharibifu unaendelea kutokana na shughuli za kilimo na ufugaji.

 

Bofya hapa kusikiliza Sauti hapa kuhusu alichozungumza mtaalam wa maji wa bonde la Ziwa Tanganyika



 

Baadhi ya viongozi wa jumuiya za watumia maji na wananchi, wameomba Serikali kuweka sheria na kuzisimamia ili kuhakikisha uharibifu huo unadhibitiwa.

 

Kwa upande wake mkuu wa Wilaya ya Uvinza Dinna Matahamani amesema kupungua mto huo, huenda miradi inayotekelezwa ikakwama na kuagiza wafugaji na wakulima kuondoka mara moja.




Miongoni mwa miradi ambayo itakuwa hatarini ni pamoja na mpango wa serikali wa kujenga mtambo wa kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto huo yaliyoko wilayani Uvinza, mradi ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni na kuchangia kupunguza uhaba na kero ya umeme mkoani Kigoma.


Bofya link hizi hapa chini ili usome kwa kina kuhusu Ziwa Tanganyika na Mto Malagarasi 


BOFYA HAPA 


Bofya hapa kuhusu Mto Malagarasi 

 

Post a Comment

0 Comments