MWANAMKE JASIRI ANAYETAMBA KWA UJUZI


 

Felister Peter Mkini ni mwanamke mwenye umri wa miaka 30, ni mmoja wa wanawake wachache tanzania waliothubutu kufanya kazi ambazo wengi hudhani ni kazi za wanaume.

Akiwa na umri wa miaka 22 alikuwa ni mmoja wa wasichana watundu waliopenda kufuatilia shughuli za uendeshaji wa mitambo ikiwemo ile ya mashambani, mitambo ya ujenzii ikiwemo inayotumika kujenga barabara kwa kiwango cha lami.

Kiu yake ya kutaka kujua mambo, hakuiacha ipite bure, taratibu alianza kufanya urafiki na wajuzi wa kazi hizo na hatimaye akakubaliwa kujifunza kazi za udereva.

Hivi sasa Felister ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Iringa ambaye pia ana makazi mkoani Arusha, anaishi mjini Kasulu mkoani Kigoma ambapo ameajiriwa na kampuni ya ZCC inayefanya ujenzi wa barabara kuu kutoka kabingo hadi Kasulu mkoani Kigoma.

Simulizi yake inasisimua, anakiri kuwa haikuwa rahisi kujifunza kazi hiyo ngumu lakini alifanikiwa kutokana na kuwa na dhamira na hamu ya kufanya kazi za udereva wa mitambo

Post a Comment

0 Comments