Mwanamke jasiri anayetamba na umahiri wa kuendesha mitambo ya Barabara

Felister Peter Mkini ni mwanamke mwenye umri wa miaka 30, ni mmoja wa wanawake wachache tanzania waliothubutu kufanya kazi ambazo wengi hudhani ni kazi za wanaume.

Akiwa na umri wa miaka 22 alikuwa ni mmoja wa wasichana watundu waliopenda kufuatilia shughuli za uendeshaji wa mitambo ikiwemo ile ya mashambani, mitambo ya ujenzii ikiwemo inayotumika kujenga barabara kwa kiwango cha lami.

Kiu yake ya kutaka kujua mambo, hakuiacha ipite bure, taratibu alianza kufanya urafiki na wajuzi wa kazi hizo na hatimaye akakubaliwa kujifunza kazi za udereva.

Hivi sasa Felister ambaye ni mzaliwa wa mkoa wa Iringa ambaye pia ana makazi mkoani Arusha, anaishi mjini Kasulu mkoani Kigoma ambapo ameajiriwa na kampuni ya ZCC inayefanya ujenzi wa barabara kuu kutoka kabingo hadi Kasulu mkoani Kigoma.

Simulizi yake inasisimua, anakiri kuwa haikuwa rahisi kujifunza kazi hiyo ngumu lakini alifanikiwa kutokana na kuwa na dhamira na hamu ya kufanya kazi za udereva wa mitambo

"Haikuwa rahisi kwangu kujua kuendesha mitambo, lakini nilikuwa ninatamani nami kuwa mjuzi wa kazi hii na nikaweka bayana hamu yangu na kisha nikapata mafunzo, kama mwanamke mwingine nilikutana na vikwazo ikiwemo kukatishwa tamaa na wanaume na hata wanawake wenzangu kuwa sita weza, lakini leo wote wanashuhudia umahili wangu" Anasema Felister

Akizungumza na Buha TV, Felister anabainisha kuwa katika kazi yake ameruka vihunzi vingi hadi kuwa mtaalamu wa kuendesha mitambo, anasisitiza kuwa wakati mwingine wanaume humdharau na kumfanyia vitendo visivyofaa lakini yeye huutumia ujasiri wake pamoja na kufuata taratibu za kazi kuepuka mitego yao.

Fuatilia simulizi yake katika video iliyoandaliwa na Buha news na Buha TV online kwa kubofya hapo chini.

Bofya Video ya Felister hapa




 

Post a Comment

0 Comments