Ndoto ya mkoa wa Kigoma na Ziwa Tanganyika kupata meli yakolea

 


SERIKALI Kupitia Wizara ya Uchukuzi, imetia Saini kwa ajili, ujenzi Meli mbili za Mizigo katika ziwa Tanganyika na Victoria miradi ambayo imeghalimu zaidi ya Bilioni 600.

Ujenzi wa Miradi hiyo unatazamwa kuwa chachu ya kuinua uchumi wa Mkoa wa Kigoma na Taifa kupia huduma za meli katika maziwa makuu hususani Tanganyika.

Katika Hafla ya utiaji saini wa mikataba mitatu Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa Profesa Makame Mbarawa ameagiza miradi hiyo kuanza haraka na ikamilike kwa wakati.


Mkuu wa mkoa wa Kigoma Mheshimiwa Thobias Andengenye amesema hatua hiyo ni dalili ya kufungua mkoa wa kigoma kuwa kitovu cha biashara

Mwakilishi wa Mkurugenzi Shirika la uwakala wa Meli Nchini TASAC Nelson Mlali akieleza kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa meli hizo kwa ufanisi.

Post a Comment

0 Comments