Prof. Aendeleza furaha kwa wapiga kura Kasulu

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Pro. Joyce L. Ndalichako Ameandaa na Kuendesha Hafla  ya Uwezeshaji wa Nishati Mbadala ya Gesi kwa mala ya Pili, Ametoa Mitungi 600 yenye Thamani ya Shilingi 42,000,000/= kwa Baba Lishe na Mama Mishe katika Jimbo lake la Kasulu Mjini Leo Alhamis 26, Octoba 2023.


Hafla hiyo imefanyika katika Ukumbi wa chuo Cha Ualimu Kasulu (TTC). Huku ikihudhuriwa na Viongozi wa chama Cha Mapinduzi CCM, Watumishi wa serikali, Waandishi wa Habari, Wadau wa Maendeleo kutoka Orxy Tanzania pamoja na Wananchi na Wakazi wa Kasulu (Mama na Baba Lishe).

Katika Hafla hiyo Pro. Joyce Ndalichako amewataka Wakazi wa Kasulu kutumia Nishati Mbadala ya Gesi na kuachana na matumizi ya Kuni na Mkaa, Kwani Nishati hiyo Safi ya Gesi inarahisisha maisha, Inamkomboa Mwanamke na Mtoto wa kike dhidi ya Adha ya kutumia Muda mwingi kutafuta kuni na mkaa, Inaokoa Muda wa akuandaa chakula vilevile  Nishati hiyo Ni rafiki kwa mazingira na Afya za watumiaji.

Mbunge wa Kasulu mjini Prof Joyce Ndalichako pamoja na mkurugenzi wa kampuni ya gesi ya Orxy wakikabidhi jiko la gesi kwa mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Izack Mwakisu (kulia) na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kasulu Comrade Mbelwa Abdallah (kushoto)
Wanamama wa Kasilu wakifu
Wajasiriamali Baba lishe na Mama lishe wa mjini Kasulu wakifurahia kukabidhiwa majiko ya gesi kutoka kwa profesa Ndalichako


Pia Prof. Joyce Ndalichako amewataka Wakazi wa Kasulu kuachana na Matumizi ya Kuni na Mkaa kuwa tayari kutumia Nishati Mbadala ya Gesi huku akiwasisitiza Kujaza Kitungi yao ya Gesi mala baada ya Mitungi hiyo kuishiwa Gesi.

 "Na mitungi ikiishiwa Gesi msiitumie Kama vigoda huko Majumbani Kwetu, tuhakikishe tunaijaza tena Gesi, tutumie Nishati ya Gesi kwani ni Bora Sana na inapika chakula kinaiva vizuri"....

 "Hata Mimi nimekuwa Mtumiaji Mzuri wa Nishati mbadala ya Gesi hasa Gesi Oryx kwa Miaka mingi Sana.. ni Gesi nzuri na salama"

Mkurugenzi wa kampuni ya Orxy akikabidhi majiko 600 ya gesi safi kwa Profesa Joyce Ndalichako 

Naye Mkuu wa wilaya ya Kasulu Mhe. Isack Anthony Mwakisu amempongeza Pro. Joyce Ndalichako kwa kuendelea Kushirikiana na kuunga mkono jitihada za Maendeleo wilayani hapo.

"Mimi binafsi nampongeza Sana Mbunge wa wetu mama Joyce Ndalichako Kwa jitihada kubwa anaiyoifanya kusaidia na Kuchangia katika Miradi ya Maendeleo ya Kasulu, Kuna wenzangu wananionea wivu wanatamani kuja kufanya Kazi Kasulu"

Ikumbukwe tu, Pro. Joyce Ndalichako amekuwa akiaandaa na Kufanya Hafla Kama hizi za Uwezeshaji katika Jimbo la Kasulu ikiwa ni pamoja na Uwezeshaji katika Sekta ya Elimu, Afya, Michezo na Nishati Mbadala ya Gesi. Utakumbuka mala ya mwisho Kuendesha zoezi la Uwezeshaji wa Nishati mbadala ya Gesi Jimboni ilikuwa mwezi Septemba mwaka huu kwa Wanawake, Shule za Msingi na Shule za sekondari  Halmashauri ya Mji Kasulu.

Jumla ya mitungi midogo 1000 ya gesi yenye majiko ya kupikia imegawiwa kwa wajasiriamali mjini Kasulu kama sehemu yanutekelezaji wa mpango wa Serikali na Rais Dr. Samia Suluhu Hassan ya kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kumtua mama kuni kichwani

Imeandikwa na Sungura, Buha Media

Post a Comment

0 Comments