Tanzania yasaini mkataba wa Bandari na kampuni ya DP World ya Dubai


 

Na. Mwandishi wetu, Ikulu Dodoma

Kampuni ya kimataifa ya Dubai Port kutoka Falme za kiarabu sehemu ya Dubai imeasaini mikataba ya kuendeleza Bandari ya Dar es Salaam baada ya kufikia makubaliano na serikali ya Tanzania kwa lengo la kuboresha huduma za bandari ili kuleta tija katika sekta hiyo.

Utiaji saini wa mikataba hiyo umefanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma mbele ya Rai wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama ChaMapinduzi (CCM) ambacho kiliahidi kufanya maboresho katika sekta za kiuchumi katika ilani yake ya Uchaguzi ya mwaka 2020/2025

Akiongea katika Halfla hiyo Ambayo imemhusisha waziari wa Uchukuzi wa Tanzania prof. Makame Mbarawa na mkurugenzi wa DP World Sultan Ahmed bin Sulayem, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema Mikataba ya Uwekezaji wa Bandari iliyosainiwa imezingatia maoni yaliyotolewa kupitia makundi mbalimbali ya kijamii, pamoja na sheria na taratibu zote za nchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na wageni mbalimbali kwenye hafla ya Utiaji saini Uwekezaji na Uendeshaji wa Sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2023.

Rais Samia amesema hayo leo wakati wa
hafla ya utiaji saini mikataba 3 ya uwekezaji katika Bandari ya Dar es Salaam kati ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), serikali na Kampuni ya DP World ya Dubai iliyofanyika Ikulu, Chamwino 

Aidha, Rais Samia amesema serikali ilisikiliza maoni mbalimbali yaliyotolewa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, vyama vya Siasa, asasi za kiraia, wanaharakati, vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, viongozi wa dini na baadhi ya viongozi wastaafu.

Vile vile Rais Samia amesema mikataba iliyosainiwa imetokana na makubaliano ya awali kati ya serikali na Mamlaka ya Dubai ambao wameridhia mahitaji na matakwa ya nchi kama yalivyoainishwa kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

Waziri wa Uchukuzi Mhe. Makame Mbarawa akiwa pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Godius Kahyarara wakitia saini Mkataba wa Nchi Mwenyeji baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kampuni ya DP World ya Dubai iliyowakilishwa na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Sultan Ahmed bin Sulayem kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2023.

Mikataba
iliyosainiwa ni Mkataba wa Nchi Mwenyeji (Host Government Agreement); Mkataba wa Upangishaji Ardhi (Lease Agreement) na Mkataba wa Uendeshaji wa Bandari (Concession Agreement). 

Rais Samia pia amesema uimarishwaji utakaofanywa kupitia uwekezaji huu utakuza biashara za ndani na nje, pamoja na kuwezesha shughuli za kiuchumi za nchi jirani hivyo kuongeza mapato ya serikali na kukuza uchumi wa taifa.

Mikataba hii 3 imesainiwa  kwa kuzingatia Kifungu cha 2 cha Sheria ya Ubia Namba 6 ya mwaka 2023 (the Public Private Partnership Act Cap 103) na Kifungu cha 2 cha Sheria ya Ununuzi wa Umma Namba 5 ya mwaka 2023 (the Public Procurement Act No 5 of 2023).

Viongozi mbalimbali wa serikali na wadau wa maendeleo akiwemo mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa mamlaka ya Bandari Tanzania balozi Ernest Mangu ambaye ni Inspekta Jenerali mstaafu wa jeshi la Polisi wameshuhudia utiaji saini huo.


Viongozi mbalimbali pamoja na wageni waliohudhuria hafla ya Utiaji saini Uwekezaji na Uendeshaji wa Sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 22 Oktoba, 2023.

Hatua hiyo imejiri miezi mitatu tangu yalipoibuka malumbano baina ya wanaharakati na serikali kuhusu makubaliano ya Tanzania na Dubai kwenye uwekezeji huo ambapo viongozi baadhi wa vyama vya upinzani na wanaharakati walipinga aina ya makubaliano yaliyokuwemo katika andiko la awali la mkataba huo, huku serikali ya Tanzania ikisisitiza kuwa dhamira yake ni njema na kuahidi kuyafanyia kazi maoni ya watanzania kuhusu makubaliano kati yake na kampuni hiyoya Bandai ya Dubai.


Post a Comment

0 Comments