TARURA Morogoro yawapiga mkwara wakandarasi


*TARURA haitosita kuwachukulia hatua wakandarasi na watumishi watakaozorotesha kasi ya  utekelezaji wa kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara za Wilaya*


Morogoro

Meneja wa Wakala ya Barabara za Vijijini  na Mijini (TARURA) mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmauel Ndyamkama amesema kuwa ataendelea kusimamia ubora wa kazi zinazofanyika katika Mkoa huo kwa kuzingatia matakwa ya mikataba inayosainiwa baina ya TARURA na Makandarasi.

Hayo yamejiri wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa Daraja la Ruhembe liliopo Kata ya Ruhembe Jimbo la Mikumi katika Wilaya ya Kilosa .



Mhandisi Ndyamkama ameeleza kuwa daraja hilo lenye  urefu wa mita 40 limefikia asilimia 80 ya ujenzi wake na kwamba hatua zote zinaendelea kufuatwa kulingana na mkataba ili likamilike na kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.

"Daraja hili kama linavyoonekana ni sehemu ya miradi inayotekelezwa katika mkoa huu, kuna baadhi ya watu wasio na nia njema wanaojaribu kupotosha juu ya jitihada hizi lakini kimsingi kazi hizi zinajionesha na ubora unazingatiwa".Amesema mhandisi Ndyamkama.

“ TARURA Morogoro haitosita kuwachukulia hatua makandarasi na hata watumishi watakaobainika kuzorotesha ama kuhujumu kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara na kwamba atahakikisha  lengo la Serikali la kutoa  huduma bora kwa wananchi  linafikiwa”Aliongeza

Kwa upande wake Bw. Hassan Salum Mwaking'inda mkazi wa Kata ya Ruhembe amesema kuwa ujenzi wa Daraja hilo utasaidia wananchi katika kuzifikia huduma za kijamii pamoja na kufanya biashara.

" Daraja hili ni mkombozi wetu maana likikamilika litatusaidia kijamii na kiuchumi hasa katika kusafirisha miwa kwenda kiwandani". Amesema Salum.

Post a Comment

0 Comments