UTEUZI: Sophia awa mshauri wa Rais, Makonda Mwenezi CCM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua ndugu Sophia Edward Mjema kuwa Mshauri wa Rais masuala ya Wanawake na Makundi Maalum.

Kabla ya uteuzi huu Bi. Sophia alikuwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM.

Wakati huo huo kamati kuu ya halmshauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM imemteua Paul Makonda kuwa Katibu wa NEC Siasa,, Itikadi na uenezi Taifa

Makonda ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Umoja wa Vijana wa CCM kabla ya kuteuliwa kuwa mjumbe wa Bunge la Katiba na baadaye nafasi ya mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mjema anayehamia Ikulu

Aidha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imemteua Rabia Abdallah Himid kuwa Katibu wa NEC siasa na uhusiano wa kimataifa.

Teuzi hizi zinakuja huku Tanzania ikijiandaa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwakani 2024 na uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais utafanyika mwaka 2025

Post a Comment

0 Comments