MULEBA DC YATWAA KOMBE NA MEDALI SHEMISEMITA

Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera imeubuka mshindi wa sita kitaifa pamoja na kupatiwa kombe na medali kwenye mashindano ya kitaifa ya shirikisho la michezo Serikali za mitaa Tanzania  Shimisemita ambayo yamefanyika Jijini Dodoma.

Akisoma taarifa ya wakati wa mapokezi ya timu ya Muleba DC Mosses Kuyella leo hii katika ukumbi wa Halamshauri ya Wilaya hiyo amesema kuwa kulikuwa na jumla ya michezo tisa na zote wameweza kuingia nane bora na nyingie kufikia hatua ya nusu fainali.



Amesema kuwa wameweza kupata kikombe cha mshindi wa tatu kwa kuvuta kamba kitaifa na kupata medali ya mshindi wa tatu wa riadha ambapo kwa kipindi cha miaka kumi timu hiyo ya muleba ilikuwa haijawahi kushiriki mashindano hayo ya kifaifa kutokana na sababu mbalimbali.

Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba Bw. Justus Magongo ameagiza  ofisi ya utamaduni kuendelea na zoezi la kutafuta wachezaji wengine ili kuwaunganisha na kuwa nguvu moja.

Post a Comment

0 Comments