OHIDE yawajengea uwezo wanawake wajasiriamali Kasulu

Asasi ya  Uwekezaji utu na maendeleo (OHIDE) yenye makao makuu mjini Kasulu mkoani Kigoma limetoa mafunzo ya haki, uchumi na mawasiliano kwa wanawake wajasiriamali wilayani Kasulu ili kuwajengea uwezo wa kutambua, fursa zinazotokana na malengo endelevu ya dunia (SDGs)

Mafunzo hayo ambayo yamefadhiliwa na Shirika la Umoja wa mataifa (UNA) nchini Finland kupitia UNA Tanzania yamefanyika kwa siku mbili mjini Kasulu ambapo wanawaje wanaojihusisha na shughuli za uchumi wa kati ikiwemo kilimo, urembo, mama lishe na wauzaji wa vinywaji (wahudumu wa Baa) wameshiriki

Akifungua mafunzo hayo Mjumbe wa Bodi ya OHIDE Bi. Jovina Mhini amepongeza na kushukuru mwelekeo wa shirika la OHIDE kwa kudhamiria kuwajengea uwezo wanawake ambao wengi ni wahanga wa ukosefu wa haki na ukandamizaji wa kijinisia


Bi. Jovina Mhini mjumbe wa Bodi ya OHIDE akitoa nasaha kwa washiriki, kushoto ni mkufunzi wa ujasiriamali kwa wanawake Bi. Anastazia Kavugushi kutoka shirika la WEGCC

Bi. Mhini ametoa shukurani pia kwa shirika la umoja wa mataifa (United Nation Association of Tanzania) pamoja na Finland kwa kutoa fedha ili wanawake wafundishwe na kujengewa uwezo katika kushiriki shughuli za umoja wa mataifa na SDG kupitia kituo cha habari cha BUHA ambayo ina kituo cha Radio, Runinga mtandaoni pamoja na mitandao ya habari kupitia internet.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa OHIDE Bi. Silesi Malli ameeleza kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha kunakuwepo na wanawake wenye kujitegemea na wanaozifahamu haki zao za kijamii.

Bi. Malli amesisitiza kuwa kadilii dunia inavyoendelea sambamba na ukuaji wa sayansi na teknolojia wanawake wamekuwa wahanga wa matatizo ya uvunjaji wa haki za kijinsia, mawasiliano hasi ya kimitandao pamoja na mbinyo wa kiuchumi katika familia na jamii kwa ujumla

Bi.Silesi Malli Mwenyekiti wa UNA Tanzania na mwasisi wa OHIDE akitoa mada kuhusu haki za wananwake na namna ya kuwasiliana na jamii kwa tija kupitia mitandao ya kijamii na Radio

"Mafunzo haya ambayo yamefadhiliwa na UNA Finland kupitia UNA Tanzania ni chachu mhimu kwa wananwake wa mkoa wa Kigoma kutumia vyombo vya habari husuasani Radio za kijamii na mitandao ya kijamii inayozingatia kanuni za uhariri kujadili masuala ya haki za vijana na wanawake

Anastazia Kavugushi alikuwa mtoa mada kuhusu fursa za kiuchumi kwa wananwake na vikwazo va kijamii vinavyowakabiri wanawake, katika mada yake Anastazia anabainisha kuwa wanawake ndio wajenzi mahili wa familia hivyo wanapaswa kuondokana na dhana potofu ya utegemezi

Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya Haki, Uchumi na Mwasiliano yaliyoendeshwa na OHIDE/BUHA MEDIA kwa hisani ya UNA Finland na UNA Tanzania

Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo akiwemo Flora Kavura, Winnie Vasco na Flora Hindanya wamekiri kuwa jamii yao inakabiriwa na changamoto nyingi na kwamba mafunzo waliyopatiwa ni mlango sahihi wa kutokea katika kupigania haki na utawala

Jumla ya wanawake na vijana ishirini kutoka Kigoma, ikiwemo Manspaa ya Kigoma Ujiji, Kasulu vijijini na halmashauri ya Kasulu mji wameshiriki mafunzo hayo ya awali juu ya Haki,, Uchumni na mawasiliano ambapo wataanza kutumika kubuni na kutengeneza maudhui ya kijamii kupitia Radio jamii kwa ajili ya jamii ya wakimbizi na wenyeji.


Uwasilishaji wa kazi za vikundi baada ya kujadiliana kuhusu hali halisi ya maisha ya wanawake na vijana

Uwasilishaji wa ubunifu wa majina ya biashara mtandaoni kama walivyojadili katika vikundi vyao


Usikose kutembelea ukurasa wetu wa Buha TV Online kupitia Youtube ili utazame matukio zaidi yaliyojili wakati wa mafunzo hayo ikiwemo uwasilishaji wa mada na mijadala ya wanawake hawa kuhusu malengo endelevu ya Umoja wa mataifa (SDGs)

Post a Comment

0 Comments