Wanaume wanaofanyiwa Ukatili wasikilizwe kama ilivyo kwa wanawake

 


Na. Editha Edward, Geita


Kumekuwepo na dhana kuwa wanaofanyiwa ukatilili ni akina mama na watoto pekee lakini imebainika kuwa kuna wimbi kubwa la  la wanaume linalofanyiwa ukatili  bila kupata msaada wa kisheria na limekuwa likisahaulika kwakuwa mila na destuli zina watambulisha kuwa watu imara.


Katika jamii za kiafrika na hata nchi za magharibi inasahaulika kuwa kitendo cha ukatili anaweza kufanyiwa mtu yoyote mwanaume  au mwanamke kwa lengo la kumdhuru ama kumuathiri kisaiklojia, kimwili, kiafya, kiakili, kingono  na kiuchumi.


Imebainika kuwa jamii zimekuwa zikiamini kuwa mwanaume nimtu imara ambaye hawezi kunyanyaswa jambo ambalo kiuhalisia sio kweli na wao ni Binadamu wanaweza kufanyiwa ukatili na kusababisha kumuasili kiakili na hata kushidwa kuendesha shughuli zake za kila siku kwa amani.


Pichani ni  Evarist Ntobi mkazi wa katoma mjini Geita yeye amekuwa akikumbwa na mikasa mbalimbali anayofanyiwa na mke wake nyumbani kwake ambapo amekuwa akimfanyia ukatili mbali mbali na akienda katika ofisi za serikali ya kijiji hapewi huduma na badala yake wanaamini kuwa mwanamke ndie anaefanyiwa ukatili.


“sikumoja nikiwa nipo kazini mwanamke alibeba kila kitu nyumbani sikujua alipo elekea baada ya siku kazaa aliludi na kwenda dawati la njisia kushitaki kuwa nimemfukuza tulishauriwa na kurudi wote nyumbani” anasimulia.


Ntobi anasema kuwa baada ya kurudi nyumbani alitoka kidogo katika shughuli zake za kawaida na mwanamke alimuacha nyumbani baada ya muda mfupi alirejea nyumbani na akaona mkewe akiongea kwa jaziba bila kufahamu kilichomsibu huku akikukusanya nguo zake wakati yeye akiwa anamusikiliza gafla mwanamke alichukua panga na kumukata sehemu za mkono.


inaelezwa kuwa mwanamke aliondoka lakini amekuwa akimutisha kwanjia ya simu kuwa tamushughulikia kitendo kinachosababisha yeye kushuka katika utendaji wake wakazi lakini ikiwemo kukosa amani kwa kuhofia kujeruhiwa na mkeo ambae kwa sasa wametengana.


Anasema kuwa anaiomba polisi pamoja na vyombo vingine kumusaidia ilikupata haki zake maana amekuwa akipata wakati mgumu na amekuwa akitoa taarifa lakini polisi hawafatilii anasema kuwa na yeye kama binadamu anaweza kuchukuwa hatua nyingine ilikujihami na yakatokea madhara makubwa zaidi.


Anasema yeye ni mfanyakazi wa shughuli za Ulinzi wa usiku na kwamba amekuwa akipokea simu na messeji kutoka kwa mkewe nyingi  za vitisho na simu nyingine hupigwa na watu tofauti asio wafahamu akitishiwa.


Anasisitiza kuwa kitendo hicho cha mke wake kumutishia humufanya akose amani na kuvitaka vyombo vya sheria kuwasikiliza wanaume wanapo peleka malalamiko yao kama wanavyofanya kwa wanawake ilikila mmoja ampate haki.


Slivestar Chigabilo ni dreva bajaji mjni Geita yeye anasema kuwa wanaume wamekuwa wakikutana na manyanyaso mbalimbali kutoka kwa wake zao wao hupambana kutafuta riziki lakini wanaporudi nyumbani hukutana na manyanyaso ya wanawake zao hasa pale wanapo kuwa na changamoto za kiuchumi.


“Unaweza kupata abiria ukaenda umbali mrefu wakati mwingine unakutana na changamoto ya mtandao unakuwa haupatikani unapoludi nyumbani unakutana na kesi za mwanamke kwa madai kuwa ulikuwa na wanawake hivyo tunaomba na sisi serikali itusaidie tusikilizwe na tupate haki kama wanavyopata wenzetu” anasema Chigabilo.

 

Slivester amaitaka serikali na viongozi wa dini kuwasaidia wanaume na kuwasikiliza anasema anaweza kupata unynyaji nyumbani anapoenda polisi huambiwa kuwa mwanaume unalalamika kitendo kinacho wafanya kuchukizwa na kujichukulia hatua ya kuwapiga wake zao na kuonekana wanawanyanyasa wake zao.


Anasema kuwa vongozi wadini wabebe jukumu la kuwaelimisha wanawake wakiwa katika nyumba za ibada ili wapate elimu ya kutoivunja ndoa na kusababisha watoto wa mitaani .


Aidha anasema kuwa wanaume ni watu wa kutunza siri kwa kuongopa kusema anayofanyiwa na mke wake kwa kuogopa kudhalilika lakini ni ukweli kwamba wanaume wanakumbana na madhila makubwa katika familia zao ila limekuwa kundi la mwisho kusikilizwa katika kutafuta haki.


Mabula Bujiku ni kazi wa Shilabela mjini Geita yeye anasema  amekuwa akishuhudia manyanyaso mengi kwa baadhi ya wanaume na wamekuwa wakikaa kimya na kushidwa kwenda kushitaki kwa hofu ya kuchekwa na wamekuwa wakijichukulia hatuwa mikononi na kuwapiga wanawake kitendo kinachosababisha watoto kushidwa kupata malezi ya baba na mama.


Anasema kuwa iwapo serikali ikitoa kipaumbele kwa wanaume kupata haki ya kusikilizwa kama wanavyofanya kwa wanawake wangetambua kuwa na wanaume wanahaki ya kusikilizwa, heshima ingekuwepo na wimbi la ndoa kuvunjika lingepungua ama kuisha kabisa na watoto wa mtaani wangepungua kwani ndoa kuvunjia ndio chanzo cha watoto hao


Jamii na serikali imetakiwa kutambua kuwa binadamu wote ni sawa na wanaume wanahaki ya kusikilizwa kwani kunawanaume wanapata ukatili mkubwa katika familia zao na hawana pa kusemea kwa hofu ya kudharauliwa na kuchekwa.


Juhudi za kuwapata wanawake waliolalamikiwa pamoja na maafisa ustawi zinaendelea na tutakuletea maelezo ya kina katika makala ijayo.


Kama una maoni kuhusu makala haya tafadhali wasilisha kupitia Barua pepe buhamedia@gmail.com au andika katika tovuti hii.

 

Post a Comment

0 Comments