Waziri aagiza zitengwe fedha kunusuru Mazingira.


NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira  Khamisi Hamza Khamisi ametaka fedha zitengwe ili kuhakikisha changamoto ya uhifadhi wa Mazingira na mapambano dhidi ya mabadiliko na athari ya tabia nchi kwani ni janga la dunia

Haya ameyasema jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya Ukusanjaji wa Mapato ya ndani kwenye sekta ya uzinduaji unavyoweza kufadhili mabadiliko ya tabia nchi ambapo Naibu Waziri huyo amesisitiza na nakuta fedha zinazokusanywa kwenye ripoti hiyo zijiekekeze kwenye kampeni za kitaifa za Mazingira kama vile  kampeni ya soma na mti.

Amesema fedha zitakapo patikana kwenye sekta ya Gesi, Nishati na Madini zielekezwe na ziendeleze kampeni za serikali zilizoanzishwa za kutunza mazingira na kukabiliana na mabadiko ya tabia nchi. 

" Nchini kwetu tatizo la uharibifu wa Mazingira lipo kwa kiasi kikubwa na hiyo yote nikutokana na uelewa mdogo kwa wananchi juu ya umuhimu wa utunzaji wa Mazingira  na ndio maana wanajikatia miti hovyo hawaliurimii taifa wao wanaamini ni jambo la kawaida ni wajibu hawakosei," Amesema. 

"Ripoti hii iende ikatoe elimu katika jamii umuhimu wa kupanda na kutunza miti na Mazingira kwa ujumla tusipo fanya hivyo vizazi vijavyo vitakuja kujua kuwa asilimia kubwa ya Tanzania ni jangwa kumbe ni kutokana na ukataji wa miti, " Amesema Naibu Waziri Khamisi

Pia ameekeza ripoti hiyo ijikite kwenye Utunzaji wa vyanzo vya maji kwani bado kuna changamoto watu wanachepusha maji wanatoa maji katika asili yake na kupeleka mashambani kwao. 

Amesema watu wamesahau sheria ya Mita 60  wanalima karibu na mito wanatumia mbolea za sumu zinakwenda kwenye vyanzo vya maji na kupelekea viumbe hai wengine kufa au kupotea  kwenye Mito. 

" Sasa Ripoti hii ihimize na kuzungumza juu ya utunzaji wa vyanzo vya maji kwani ukweli ni kwamba Mito ni maisha yetu, " Amesema. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Policy Forum Christina Ruhinda amesema wanachama wa Policy Forum wapo kwenye taasisi mbilimbali ambazo zinashughulikia masuala yanayohusu sekta zote hapa nchini. 

Mwenyekiti wa Policy Forum Christina Ruhinda

Amesema wanachama wanagusa mipango yote na kushikili katika utekelezaji ili kuhakisha Tanzania inafikia maendeleo yaliojipangia kimkakati kuyafikia na kuchangia katika ukuaji na kuhakisha uwajibikaji na ufanyaji kazi kwa watu wote. 

Naye Makupa Nsenduluka Afisa Sera Kodi na Usimamizi wa Rasilimali amesema kama ilivyo kwa nchi nyingi zinazoendelea, Tanzania imeathiriwa Sana na mabadiliko ya tabianchi madhara ambayo hayaishii tu kusababisha mafuriko na ukame lakini yanaharibu Miundombinu na hata kuathiri maisha ya watanzania. 


Imeandikwa Na Jasmine shamwepu Dodoma

Post a Comment

0 Comments