CCM na SWAPO wakutana Dar es Salaam kuteta jambo

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdurahman Kinana amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Chama Cha SWAPO cha Namibia Komredi Sophia Shaningwa, Disemba 08, 2023, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba, jijini Dar es Salaam.


Chama Cha Mapinduzi kimekuwa na desturi ya kukutana na viongozi waandamizi wa vyama vya siasa vilivyopigania uhuru barani Afrika pamoja na vyama rafiki vya China na Cuba.

Utamaduni huu unatajwa kuwa moa ya nyenzo za kuwa chama makini na chenye nguvu kilichobaki madarakani baada ya kuanzishwa kwa vyama vingi.


Post a Comment

0 Comments