Dr. Biteko awataka wahitimu kuhudumia watu wa hadhi zote.


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Dotto Biteko akisalimiana na Mhashamu Baba Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga - Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Mbeya, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino cha Tanzania na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania(TEC) kabla ya kufanyika kwa Mahafali ya 26 ya SAUT.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wahitimu wa Vyuo mbalimbali nchini mara baada ya kupata ajira kuwahudumia watu wa makundi yote hasa ya maskini kwani kila mwananchi ana haki ya kupata huduma bora bila kujali hadhi aliyonayo.

Amesema hayo katika Mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu cha MtakatifuAugustino cha Tanzania (SAUT), tarehe 16 Desemba 2023 yaliyofanyikak atika Viwanja vya Raila Odinga jijini Mwanza.

"Ndugu wahitimu na wale ambao tupo kazini, tusikilize watu wa makundi yote hasa wale wasio na kitu cha kutulipa na tuone fahari ya kunyanyua hadhi ya watanzania kwenda kwenye maisha yaliyo bora zaidi kwani ukisaidia maskini unakuwa umesaidia wananchi wengi zaidi."Amesema Dkt. Biteko

Aidha, Dkt. Biteko ametaka wahitimu nchini kuchukia rushwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi kwakuwa ni chanzo cha kuwanyima haki watu wasio na uwezo.

Dkt. Biteko amesema, Serikali itaendelea kuweka mazingira mazuri na wezeshi kwa kila mtu mwenye juhudi na kuhakikisha kwamba mazingiraya kufanya kazi yanakuwa bora.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt.Dotto Biteko akisalimiana na Viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Mahafali ya 26 ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini Mwanza leo.

Kwa upande wa makamu Mkuu wa Chuo cha SAUT, Profesa Costa Ricky Mahalu, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Awamu ya Sita, kwa kuvisimamia na kuviendeleza vyuo vikuu nchini ambavyo vimeendelea kuzalisha wahitimu wa kada mbalimbali na kwa ushirikiano mzuri ulipo kati ya Serikali na Chuo hicho ambao umepelekea kupata wanafunzi wa kutosha kila mwaka.

Katika Mahafali hayo Jumla ya wanafunzi 3,066 wamehitimu masomo yao katika ngazi mbalimbali ikiwemo Shahada ya Uzamivu katika Mawasiliano ya Umma, Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara, Shahada ya Uzamili ya Uchumi na Shahada ya Uzamili ya Sheria.

Mwandishi: Teresia Mhagama.

Post a Comment

0 Comments