Shahada nyingine ya heshima yatolewa kwa Dr. Samia

Rais Samia Suluhu Hassan atunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi wa Utalii na Masoko katika Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Tunguu Zanzibar.

Hafla hiyo ya aina yake ambayo imeenda sambamba na kuwatunuku wasomi wengine waliomaliza na kufaulu masombo katika fani mbalimbali ndani ya Chuo Kikuu cha Zanzibar yamefanyika leo huko Unguja Zanzibar


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine akiwa kwenye maandamano ya Kitaaluma wakati walipokuwa wakiingia kwenye Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu kwa ajili ya kushiriki Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) 


Chuo hicho kimemtunuku Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake wa kuifungua nchi kiuchumi kupitia Sekta ya Utalii ambapo kupitia filamu yake ya The Royal Tour tanzania imerekodi wageni wengi zaidi wanaokuja kufanya shughuli za utalii na biashara


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Aman Abeid Karume katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu walipohudhuria Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) mapema leo.


soma zaidi maoni na coment za watu kwenye X


bofya hapa


Rais Samia anaandika Historia ya kuwa Mwanamke wa Kwanza Rais katika nchi za Afrika mashariki na rais wa tatu Barani Afrika na shahada aliyipewa ni ya pili baada ya ile ya Udaktari aliyotunukiwa na chuo kikuu cha Dar es Salaam


Imeandikwa na; Amour Kassim-Ikulu

Imehaririwa na: Prosper Kwigize

Post a Comment

0 Comments