Na. Editha Edward, Geita
WAZIRI wa maendeleo ya jamii,jinsia wanawake na makundi maalum Dkt. Dorodhi Gwajima amesema vitendo vya ukatili hugharimu uchumi wa nchi na dunia kwani fedha nyingi hutumika kutoa huduma kwa jamii iliyoathiriwa na matukio ya kikatili.
Dkt Gwajima amesema hayo wakati akifunga tamasha la maendeleo mkoani Geita lililoenda sambamba na kutoa elimu ya kupinga ukatili kwa jamii,ambapo amesema serikali ya tanzania ni miongoni mwa nchini duniani zinazotumia fedha nyingi kuhudumia jamii iliyokatiliwa.
Alisema kuwa siyo lahisi kuepuka ukatili bila kushirikiana na upatikanaji wa haki katika makundi maalumu kwa kushirikiana na wizara mama yawatu wenye ulema iliyochini ya ofisi ya waziri mkuu kuhakikisha wanawezeshwa ilimakundi hayo yanufaike.
Matalajio ya mh. Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hasan nikuhakikisha sekta zote zinaungana zikiwemo sekta binafsi kuhakikisha wanafikia matalajio ya Kuzijua frusa na kukataa ukatili kwani ukatili nijanga kubwa kwa taifa na dunia kwa ujumla na kugalimu uchumi wa dunia.
“Asilimia kubwa wanaofanyiwa ukatili niwanawake na watoto wanafanyiwa ukatili hasa watoto hufanyiwa ukatili na baba zao kwa asilimia kubwa hivyo tubadilike tuepukanae na ukatili huludisha maendeleo nyumba na kudidimiza uchumi wanchi fedha ambazo zingefanya maendeleo huelekeezwa kwenye masuala ya ukatili ”alisema Dr Gwajima.
Kwajima aliwataka wananchi kujishughulisha kwani asilimia kubwa ya ukatili hutokana na uchumi duni husababisha ukatili kwa akina baba anapo kuwa hana kipato humusababishia hasira za bila sababu na kupelekea kufanya ukatili bila kutalajia.
Kwa upande wake naibu katibu mkuu wizara ya maendeleo ya jamii,jinsia,wanawake na makundi maalum wakili amon mpanju amesema njia pekee ya kuepukana na ukatili ni kuondoa ukatili kwa makundi yote ya jamii bila kujali jinsia.
Alisema kuwa lengo lakufanya tamasha la ukatili nikuhakikisha ujumbe unawafikia wananchi kupambambana na janga laukatili na kuwaasa akina baba kuepuka ukatili unapofanya ukatili katika familia unaikomazaa familia yako wataishi katika ukatili mwisho wasiku utakatiliwa wewe mwenyewe.
“Hivyo basi nawaasa wana Geita na watanzania kwa ujumla tuepuke ukatili kwa wanawake na watoto tuwena familia bora tuheshimiane wenyewe kwa wenyewe wanaume wawaheshimu wanawake na wanawake wawaheshimu wanaume pamoja na watoto”alisema
Awali akisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa wa Geita,katibu tawala wa mkoa huo Mohamed Gombati amesema matukio 343 ya ukatili yameripotiwa mkoani Geita .
Mkuu wa mkoa huo martine shigela alisema tamasha hilo limetangaza fursa nyingi za kiuchumi za mkoani lakini pia wananchi na wadau wameendeleo wameweza kujifunza na kuwa nauelewa juu ya suala la ukatili.
Aidha baadhi ya taasisi zimeshiriki kutoa huduma bure kwa jamii ikiwemo hospitali ya rufaa ya kanda ya bugando iliyopo jijini mwanza chini ya usimamizi wa afisa uhusiano wa hospitali hiyo Evelyne Mahalu.
0 Comments