Takribani watu 63 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 90 kujeruhiwa kutokana na
mafuriko na maporomoko ya udongo katika eneo la Katesh wilayani Hanang mkoani
Manyara nchini Tanzania.
Tukio hili la kutisha
limetokea jana jumapili kufuatia mvua nyingi zinazoendelea kunyesha katika maeneoo
mbalimbali nchini humo ambapo inaelezwa kuwa mamia ya makazi yameharibiwa, na
watu kukosa sehemu za kujistili na miundo mbinu mingi kuharibika ikiwemo Barabara
katika kanda ya kaskazini hususani mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, na Manyara.
Waliojeruhiwa wamekuwa wakipatiwa huduma
mbalimbali za kibinadamu ikiwemo matibabu na kuruhusiwa hali zao zinapokuwa zimeimarika na
wengine wamekuwa wakipelekwa hospitali kwa ajili ya kupata matibabu Zaidi kwa waliojeruhiwa vibaya.
Taarifa zinasema kuwa chanzo cha janga
hiyo kwa mkoa wa Manyara ni mvua nyingi zilizopelekea kuporomoka kwa sehemu ya
Mlima Hanang ulioko Jirani na mji wa Kateshi ambao
sehemu yake kubwa imekubwa na athari zinazotokana na mafuriko ya tope,
maporomoko yam awe na maji mengi katika makazi ya watu na vituo vya huduma za
umma.
Akizungumza na wanahabari, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen
Sendiga amesema eneo kubwa lililoathirika na mafuriko hayo ni kata ya Gendabi
katikati ya mji wa Katesh.
Kikosi cha kupambana na maafa chini ya Ofisi ya Waziri mkuu
kimetumwa Katesh kufanya shughuli mbalimbali za uokoaji ambapo tayari kambi
tatu zimeandaliwa kwa ajili ya kuwapatia hifadhi watu waliokosa kabisa mahali
pa kuishi.
Kufuatia janga hilo
Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan ambaye yuko Dubai
kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa mazingira COP, ametuma salaam za rambirambi kwa
wananchi wa Hanangi Pamoja na kutoa maelekezo kwa wizara zote za kisekta
kushughulikia changamoto hiyo.
Tayari Mawaziri
kadhaa wamewasili Hanang kuongoza wananchi kuwasaka wahanga wa mafuriko hayo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na
Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa, pamoja
na Wakuu wa Vyombo vya ulinzi na Usalama wamefika katika kijiji cha Gendabi
kata ya Gendambi Wilaya ya Hanang mkoani Manyara eneo yalipotokea mafuriko
ambayo yamesababisha vifo vya watu, majeruhi na uharibifu mkubwa wa Miundombinu
mbalimbali, yakiwamo mashamba na makazi ya wananchi.
Mapema leo Viongozi
hao wameongozwa na Mkuu wa Mkoa Manyara, Queen Sendiga kufika katika Kijiji cha
Gendabi ambalo ni eneo lililoathirika sana na Maporomoko ya Matope kutoka Mlima
wa Hanang yaliyotokea usiku wa kuamkia tarehe 03 Disemba 2023.
Waziri MKUU Kassim majaliwa muda mfupi uliopita naye amewasili mkoani
manyara ambapo amekagua shughuli za uokoaji na urejeshaji wa hali katika maeneo
yaliyoathirika na kuwahimiza viongozi wa mkoa na wizara kushughulikia kila
changamoto itakayoibuka kutokana na janga hilo
Aidha ametangaza kuwa serikali itagharimia mazishi kwa marehemu wote
sambamba na kutoa huduma zote kwa wahanga ambao wamelazimika kuwa wakimbizi
katika meneo yao kufuatia kubomoka kwa nyumba zao.
Wakati huo huo Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, amewahakikishia wananchi
wilayani Hanang Mkoa wa Manyara hususan waliokumbwa na janga la mafuriko,
kwamba maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, yatatekelezwa kikamilifu na idara
na taasisi zote kama walivyoagizwa chini ya usimamizi wa Waziri Mkuu
Kinana ameyasema hayo leo Desemba 4, 2023 alipowatembelea
waathirika wa mafuriko hayo katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Hanang.
Kinana amewatembelea na kuwafariji wananchi waliopoteza ndugu
zao na waliojeruhiwa na kulazwa hopitalini kutokana na janga hilo ambapo
amewapa pole na kuwaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu
wanachopitia.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana,Akiwapa pole Wakazi wa Kata ya Gendambi alipowatembelea waathirika wa mafuriko hayo katika baadhi ya vijiji vya Wilaya ya Hanang.
0 Comments