Breaking News - Rais Samia amtumbua kigogo mwingine


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Bw. Michael Songora Mjinja, Kamishna wa Petroli na Gesi – Wizara ya Nishati.

Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu ilibainisha hayo usiku wa kuamkia leo, kuwa rais wamefanya utenguzi huo, hata hivyo hakuna sababu zilizotajwa katika taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ya Ikulu inaeleza kuwa Bw. Mjinja atapangiwa kazi nyingine.

Huu ni uamuzi wa kwanza wa Rais kutengua uteuzi kwa mwaka 2024 na kumfanya Bw. Mjinja kuingia katika rekodi mbaya kwa mwaka huu.


Post a Comment

0 Comments