Chongolo apata mrithi CCM



Aliyewahi kuwa kiongozi wa jumuiya ya vijana wa Chama Cha Mapinduzi na baadaye kuwania uteuzi kuwa mgombea wa nafasi ya Urais kipitia CCM, Emmanuel Nchimbi ametwuliwa kuwa Katibu mkuu mpya wa chama hicho.

Bw. Nchimbi ametangazwa kushika wadhifa huo leo na mwenyekiti wa CCM Dr. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nchimbi ni miongoni mwa wanasiasa machachali ambaye pia ameshika nyadhifa mbalimbali ndani ya serikali ikiwemo Ubalozi.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Samia Suluhu Hassan, akizungumza jambo na Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Emmanuel John Nchimbi mara baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo kwenye Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.chimbi

 

Katibu Mkuu mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndugu Emmanuel John Nchimbi akizungumza kwa mara ya kwanza mara baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo kwenye Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilichokutana tarehe 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.


Kikao Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kilikutana tarehe 15 Januari, 2024 Mjini Unguja Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments