Wakati Vijana wa CCM wakikutana mkoani Kigoma kujadili mstakabali wa taifa, Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango amewaasa vijana kutumia vizuri mitandao ya kijamii huku akiwaonya kutokukubali kutumiwa kisiasa katika kuchochea vurugu kwa kushirkii kwenye maandamano na vurugu sisizo na tija
Aliyasema
hayo katika kongamano la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan na maadhimisho ya
miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) yalifanyika kitaifa hapo
jana katika viwanja vya Kawawa vilivyopo manispaa ya Kigoma Ujiji
"Vijana
mnapaswa kuwa kielelezo cha uadilifu, mlinde mila na desturi, mtumie mitandao
ya kijamii kuongeza maarifa ili kuleta tija na utatuzi juu ya masuala
mbalimbali katika jamii na si kutumia mitandao kuchafuana,kupotosha, na kuleta
taharuki katika jamii" Amesema Mpango.
Dkt Mpango
aliwasisitiza vijana kutumia majukwaa rasmi ya kufikisha maoni yao kwaajili ya
kupata suluhu na si kuandamana kwani maandamano sio suluhu kwa kila kitu.
"Uchumi
wa dunia umeathirika na ugonjwa wa Covid 19, Vita vya pamoja na vita
vinavyoendelea ukanda wa Mashariki ya kati, athari hizi haziwezi
kutatuliwa kwa mara moja tena kwa maandamano , vijana msikubali kutumika'
Alisisitiza Mpango
Alisema
Rais Samia anataka usawa na watu wote waheshimiane, wawe wastahimilivu na
kuepuka migogogro na pale inapobidi suluhu itafutwe mara moja ili kuleta
mageuzi ya kukuza nchi na kwamba nchi inaendelea kupambana kwaajili ya kutatua
changamoto zilizopo
Kwa upande wake Mkuu wa mkoa kamishna generali wa zimamoto mstaafu Thobias Andengenye amemshukuru Rais Samia kwa kutimiza ahadi yake ya kufungua mkoa wa Kigoma katika ziara aliyoifabya Oktoba 2022kwa kufanya kuwa kitovu cha biashara ambapo kwa kipindi cha miaka mitatu mkoa umepokea trilioni 11.450 zilizoelejezwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo
"Kwanza
Kuna mradi wa umeme katika mto Malagrasi eneo la Igamba lenye kw 45.6,
kuunganisha umeme mkubwa kutoka Rusumo, kuanzia Nyakanazi mpaka Kidahwe
takribani kilomita 280, umeme wa msongo KV 400 utatoka huko mpaka Kigoma, na
unatarajiwa kukamilika mwezi wa nne mwaka huu, mradi wa SGR kutoka Tabora wenye
urefu wa kilomita 506, kujenga reli ya Uvinza -Msongati wenye gharama ya
tririoni 1.74, kukarabati meli ya mafuta ya Mv Sangara, na ujenzi wa meli
za mizigo, ujenzi wa kiwanda cha kutengenezea meli pamoja na kudumisha huduma
za afya" Alisema Andengenye.
Naye Rehemu Sombi makamu mwenyekiti wa UVCCM alisema serikali ya awamu ya sita imekuwa kinara cha demokrasia kwa kuimarisha na misingi ya utu, kuhimiza haki, usawa na uongozi bora jambo ambalo linadumisha amani na mshikamo wa taifa letu.
"Juzi
chama ndugu kimojawapo kuliweza kufanya maandamano ambayo kipindi cha nyuma
hayakuweza kuruhusiwa lakini wamepewa ulinzi wa kutosha, na hii inaonesha
kuwepo kwa ukomavu ya kidemokraisa, iliyohuishwa katika awamu hii ya
uongozi" alisema Sombi.
Awali viongozi wa jumuia ya vijana ya CCM taifa walifanya ziara katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kufanya mikutano katika wilaya zote za mkoa wa Kigoma.
0 Comments