Kujali wanyonge ndio uongozi wanaoutaka watanzania - Ndalichako

Wakati watu wengi hususani viongozi wakikaa maofisini kusubiri kupokea malalamiko, waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, vijana na wenye ulemavu Prof. Ndalichako anahimiza viongozi kutatua kero za jamii kwa vitendo

Hayo ameyabainisha hivi karibuni alipotembelea na kuzungumza na wazee, wanawake na vijana katika kata za Murufiti na Ruhita katika jimbo la Kasulu mjini ambapo yeye ndiye mbunge wa jimbo hilo

Akizungumza na wazee hao na kisha kutoa zawadi kwa akina mama, Profesa Ndalichako ameweka bayana kuwa uongozi ni kuonesha njia kwa kufanya kazi kwa vitendo na kutatua kero na shida za wanyonge

Profesa Joyce Ndalichako akitoa zawadi ya mwaka mpya kwa wanawake wazee katika kuutambua mchango wao kwa taifa na jimbo la Kasulu. Hii ni mara ya kwanza kwa Mbunge kuwakumbuka wanawake na bibi zetu

Prof. Ndalichako amekuwa akisisitiza juu ya uongozi unaoacha alama kwa umma akiamini kuwa jamii inayo haki ya kunufaika na uongozi bora na siasa safi badala ya kuzingatia maslahi ya mtu mmoja mmoja.

Hivi Karibuni aligawa majiko ya gesi kwa ajili ya kaya masikini, mama na baba lishe kwa nia ya kuunga mkono dira ya Rais Samia ya kumtua mama kuni kichwani sambamba na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Profesa Ndalichako akicheza nakufurahi na akina mama wazee katika kijiji cha Murufiti kata ya Murufiti halmashauri ya Mji Kasulu, alipotembelea na kuzungumza na wazee

Aidha Ndalichako katika jimbo lake alitoa Cherehani kwa vikundi vya vijana waliojiajili katika fani ya ushonaji ili kuwajengea uwezo na kuwaongezea zana za kazi kwa ajili ya kuinua kipato chao.

Huu ndio uongozi unaofaa na unaoacha alama kwa wapiga kura

Imeandikwa na. Prosper Kwigize






Post a Comment

0 Comments