Jumuiya ya umoja wa Vijana wa CCM imetoa tuzo maalum kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan baada ya kutambua mchango wake katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi
Tuzo hiyo ya Ngao ya heshima imetolewa leo mkoani Kigoma na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana taifa Mohsmed Kawaida wakati wa kongamano la kitaifa la kumpongeza Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi taifa
Comrade Kawaida amebainisha kuwa Rais Samia amefanya mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo kuongeza bajeti katika kilimo, Afya, Elimu na Miundombinu
Pamoja na utendaji uliotukuka Umoja wa Vijana umemtaja Rais Samia kama Rais anayejibainisha kwa kusimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayoleta matokeo kwa jamii moja kwa moja.
Pamoja na Ngao, UVCCM imetoa kiasi cha Sh. Milioni moja kwa ajili ya kumchangia Dr. Samia Suluhu Hassani kulipia fomu ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2025.
Akipokea tuzo hiyo kwa niaba ya Rais Samia, Makamu wa Rais Dr. Philp Mpango amewapongeza Umoja wa vijana kwa kutambua mchango Rais Samia katika kuijenga Tanzania kwa manufaa ya wote.
Dr. Mpango amesema vijana wanao wajibu wa kuilinda nchi na kuhakikisha amani inadumishwa kwa kujiepusha na uchochezi na maandamano.
Amesisitiza kuwa serikali chini yabRais Dr. Samia Suluhu Hassan inahakikisha kunakuwepo na mazingira wezeshi kwa kila mwananchi kufanya kazi.
Sambamba na kongamano hilo, vijana na wana CCM wengine wamefanya maandamano ya takribani kilometa 7 kama sehemu ya kumpongeza Rais Samia kwa utendaji na uwajibikaji wake.
Kongamano maalumu la vijana kwa ajili ya kupongeza miaka mitatu ya Rais Samia Suluhu Hassan limefanyika Ujiji Kigoma likienda sambamba na kikao cha Baraza kuu la UVCCM na tafakuri ya miaka 47 ya Chama Cha Mapinduzi
Kabla ya kongamano hilo wajumbe wa baraza la vijana walifanya ziara katika wilaya zote za mkoa wa Kigoma na kukagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati ikiwemo ukarabati wa Meli ya MT Sangara naV Liemba katika Bandari ya Kigoma.
0 Comments