Breaking News: Rais Samia atengua na kuteua usiku huu

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. James Peter Mataragio kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati.

 

Dkt. Mataragio aliwahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na anachukua nafasi ya Bw. Athumani Selemani Mbuttuka ambaye uteuzi wake umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine.

Taarifa hii ni kwa mujibu wa kurugenzi ya habari na mawasiliano ya Rais Ikulu ambayo imetolewa usiku huu February 21, 2024


Post a Comment

0 Comments