Prof. Ndalichako akabidhi magari ya idara ya Afya Kasulu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye ulemavu Profesa Joyce Ndalichako ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kasulu mjini Mkoani Kigoma, amekabidhi magari mawili kwa ajili ya huduma za afya mjini Kasulu.

Akikabidhi magari hayo mapema jana katika kituo cha afya Kiganamo, Prof. Ndalichako amebainisha kuwa gari moja ni kwa ajili ya wagonjwa na jingine kwa ajili ya shughuli za utawala na uratibu katika halmashauri ya mji Kasulu

Profesa Ndalichako amemshukuru rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa magari hayo na kukiri kuwa ukosefu wa miundombunu ya afya hasa usafiri lilikuwa ni changamoto kwa jimbo lake na amekiri kuwa sasa utoaji wa huduma na ufuatiliaji umerahisishwa














"Namshukuru sana Mheshimiwa Rais samia Suluhu Hassan, amekuwa na moyo wa kuhakikisha afya ya jamii inaimarika sana, na kwa jimbo langu la Kasulu mjini ametutendea makubwa sana ikiwemo ujenzi wa zahanati mpya, vituo viwili vya afya na sasa ametoa magari mawili kwa ajili ya kuhakikisha kila idara inaimarika" alisisitiza Prof. Ndalichako

Wakati huo huo watu wenye ulemavu wapatao 20 wamenufaika na misaada mbalimbali ikiwemo viti mwendo na fimbo za kutembelea kama sehemu ya kuwasaidia kumudu maisha yao ya kila siku.

Msaada huo ulioambatana na fisaa Tiba kwa kituo cha Afya Kiganamo na hospitali ya mji ya Mlimani Kasulu, umetolewa na Mbunge Profesa Joyce Ndalichako katika hafla ya utoaji wa vifaa hivyo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na Chama Cha Mapinduzi.














Akikabidhi misaada hiyo kwa watu wenye Ulemavu pamoja na kwa mganga mkuu wa halmashauri ya Mji, Profesa Ndalichako ameeeleza kuwa, amekuwa akipokea maombi mengi ya watu wenye uhitaji hasa wazee na wenye ulemavu kuhusu zana za kutembelea na amefanikiwa kupata vichache na kwamba juhudi za kuwasaidia wengi zaidi zinaendelea



Kuhusu Vifaa tiba mbunge huyo Aidha Mhe. Ndalichako amekabidhi mashuka mapya ya kisasa 200 kwa ajili ya wagonjwa pamoja na vifaa vya kuingizia dawa mwilini kwa njia ya sindano maarufu "Kanyura" 














Pamoja na mambo mengine alikagua utoaji wa huduma katika Wadi ya wazazi na kutoa zawadi ya pesa taslimu kiasi cha shlingi 650,000 kwa wahudumu na wauguzi wa kituo cha afya Kiganamo baada ya kujiridhisha kuwa wanatoa huduma kwa weledi.

Imeandikwa na; Prosper Kwigize

Imehaririwa na: Adela Madyane


Post a Comment

0 Comments