Katika ziara hiyo iliyofanyika mwishoni mwa juma lililopita, sambamba na mambo mengine viongozi na wajumbe walitembelea na kupata maelezo ya ukarabati wa meli za MV Liemba na MT Sangara inayosafirisha mafuta kwenda katika nchi jirani
Akizungumza baada ya kutembelea bandari hiyo, Mwenyekiti wa UVCCM Comrade Kawaida amekiri kuridhishwa na mipango ya serikali kupitia wakala wa meli tanzania kwa kutenga pesa kwa ajili ya kukarabati meli hizo huku akiweka bayana kuwa uwepo wa meli ya MT Sangara ni sehemu ya ukuzaji wa uchumi wa tanzania na nchi jirani na kudumisha diplomasia
Kawaida amesisitiza kuwa Ziwa tanganyika ni kiungo mhimu kwa uchumi wa nchi za maziwa makuu hsa Zambia, DRC, Burundi na Rwanda kutokana na kuwa sehemu ya usafiri na usafirishaji wa shehena ya mizigo kutoka Bandari za bahari ya Hindi kupitia reli ya Kati hadi katika nchi hizo ambazo hazina bahari.
Kuhusu ukarabati wa meli kongwe Duniani ya MV Liemba, Comrade Kawaida ameweka bayana kuwa ni mhimu kuikarabati na kuirejesha kazini badala ya kuiegesha na kuwa sehemu ya makubusho akisisitiza kuwa endapo itafanya kazi itakuwa na faida mara dufu kama kivutio cha utalii na pia kusafirisha abiria na mizigo
Meli ya MV Liemba imekuwa ikitegemewa kwa shughu;li za usafiri na usafirishaji katika ziwa Tanganyika kwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na imesalia kuwa ni meli kongwe pekee dunaiani ambayo bado inafanya kazi licha ya kuwa na umri mkubwa
Mwenyekiti wa UVCCM Muhamed kawaida amekiri kuwa kitendo cha Tanzania kuitunza na kutenga fedha za kuifanyia matengenezo mara kwa mara ni cha kupongezwa kutokana na umhimu wa Meli hiyo katika ukanda wa maziwa makuu
"Meli hii ina historia kubwa kwa uhuru na uchumi wa nchi yetu, inatukumbusha utawala wa ukoloni wa wajerumani na waingereza lakini pia inachochea diplomasia baiana ya nchi zetu, hivyo uamzi wa kuikarabari na kuirejesha kazini MV Liemba ni busara kubwa zaidi kuliko kuiacha kuwa ghofu la makumbusho" Alisisitiza Kawida
kwa upande wake Meneja wa wakala wa Meli Kigoma Bw. Allan Butembero alibainisha kuwa Serikali kupitia wakala wa Meli nchini imetenda kiasi cha shilingi bilioni 600 kwa ajili ya kufanya maboresho ya huduma za meli nchini ikiwemo katika eneo la maziwa makuu yaani Victoria, Tanganyika na Nyasa.
Amebainisha kuwa mradi wa ukarabari wa MT Sangara ambao upo katika hatua za mwisho sambamba na miradi mingine ya maboresho katika bandari ya Kigoma utagharimu kiasi cha sh, bilioni 19 ambazo zimetolewa na serikali ili kuboresha huduma za usafiri na usafirishaji katika ziwa tanganyika na kuunga mkono usafirishaji kupitia reli ya kati.
Meli ya MT Sangara inayofanyiwa ukarabati mkubwa katika bandari ya Kigoma
Bw. Butembero ameweka bayana kuwa katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi, serikali imeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa meli mpya itakayotoa huduma katika ziwa Victoria kati ya Tanzania, Kenya na Uganda na kwamba mradi huo utagharimu kiasi cha shilingi bilioni 113.Miradi mingine ni maboresho ya cherezo cha kutengenezea meli katika ziwa tanganyika ambacho kinategemea na nchi za Burundi na DRC pamoja na kiwanda cha kuundia meli mkoani Kigoma.
Meneja wa wakala wa Meli Tanzania katika maziwa makuu Bw. Allan Butembero (mwenye suti nyeusi) akitoa maelezo kuhusu miradi ya uboreshaji wa huduma za meli nchini Tanzania hususani katika bandari za Kigoma, Mwanza na Nyasa
Meli nyingine zinazotoa huduma katika ziwa tanganyika ni pamoja na MV Mwongozo ambayo pia imekuwa ikitumika kwa shughuli za utafiti wa mafuta katika ziwa Tanganyika
0 Comments