Acheni kutelekeza watoto wenu, epukeni ukatili - UMAKI Bukoba


Umoja wa Wanawake wa kanisa la Anglikana (UMAKI), Dayosisi ya Rweru Mkoani Kagera umeeleza kusikitishwa na baadhi ya wazazi wanaotelekeza familia zao nakupelekea ongezeko la wimbi la watoto wa mitaani mkoani humo.

Hayo yamesemwa  Machi 11 2024 na viongozi wa UMAKI walipotembelea kituo cha kulelea  watoto yatima cha E.L.C.T TUMAINI CHILDREN CENTRE kilichopo Manispaa ya Bukoba na kinachomilikiwa na kanisa la kiinjili la Kilutheri  la  Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kasikazini Magharibi Usharika wa kanisa kuu Bukoba,

Makamu Mwenyekiti wa kanisa la Anglikana Parishi ya Bukoba  Irene Devid Mwananugu amesema kuzagaa kwa watoto mitaani mjini Bukoba pamoja na matukio ya ukatili dhidi ya watoto ni matokeo ya kaya kutojali na kuwajibika katika maelezi ikiwemo utelekezaji wa familia.

Bi. Mwananungu ameitaka Jamii nzima kubadilika na kuacha tabia ya kufanya vitendo vibaya kama kupiga watoto,kumpiga mwenza,kutishia kuua na  kutelekeza familia zao kwasababu wanahatalisha ndoto za baadhi ya watoto ambao hawana hatia bali nitegemeo taifa leo.

"Niseme ukweli sisi wanawake wa kanisa la Anglikana tunachukizwa na vitendo vya baadhi ya watu waosababisha mitafaruko kwenye familia nakusababisha watoto kutoroka na kukimbilia mtaani hiyo nibaya maana tunawapoteza watoto wenye ndoto kubea ya kuwa viongozi na wasomi mbali mbali" amesema Irene

Pamoja na mambo mengine wanaumoja wa wanawake UMAKI wamefanya maombi na kutoa zawadi mbalimbalikwa watoto wanaoishi katika kituo hicho, na kutoa wito kwa jamii na makundii mbalimbali kuwajali watoto hao

Zawadi mbalimbali zikitolewa kwa watoto wanaolelewa na kusoma katika kituo cha Tumaini Bukoba mkoani Kagera. Picha na Zawadi Paschal

Sister Adventina Kyamanywa ni Kiongozi wa  kituo hicho cha watoto ya Tima  cha E.L.C.T TUMANI CHILDREN CENTRE amesema kituo hicho kilianzishwa mwaka 2013 kwa lengo la kusaidia malezi kwa watoto wanaoishi mazingira hatalishi yaani mtaani na tangu mwaka huo kimesaidia kulea watoto 2000 ambao wamehitimu elimu na vyuo mbali mbali na watoto wanaopokelewa mahala hapo niwale wanaookotwa au kupatikana katika mazingira hatarishi na kituo kina uwezo wa kupokea watoto 60 na kwasasa kina watoto 56 wakike 20 wakiume 36 wote wanaishi kituoni hapo.

"Watoto tunawakusanya kutoka huko kwenye mazingira hatarishi na kuwaleta kituoni kweli kwa ajili ya kulejesha imani, makuzi, malezi, na Elimu na kituo kinapata ufadhili kutoka Sweden tangu kilipofungukiwa ila changamoto kubwa kuna baadhi ya vitu wafadhili hawatupatii kama chakula, elimu na Madharadhi hivyo tunawategemea wasamalia wema kama nyie mnapotuletea Misaada na zawadi" ameeleza Adventina 

Imani Viani nikijana wa kiume mwenye (27) ni miongoni mwa Watoto wanaishi katika kituo hicho aliletwa kutoka mtaani baada ya kuteswa na baba na Mama akaamua kikimbilia ntaani amesema kuwa anashukuru uongozi wa kituo  kuendelea kuwalea wadogo zake na kuwaona kama watoto wao wa kuzaliwa maana mara nyingi wingi wao waliyopo hapa niwale waliyokata tamaa ya maisha hivyo wanapoona jamii inawakumbuka na kuwafariji wanajihisi vizuri.

Katika Hatua nyingine Askofu mkuu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Rweru Mkoani kagera Askofu Godfrey Mbelwa amesema wao kama kanisa wataendelea kushirikiana na jamii kuendela kuwatunza watoto waliyopo kituoni hapo kwa kadili watakavyoweza na amewaomba watu  mbali mbali wenye uwezo kuzidi kujitokeza katika kunusuru watoto hao maana watoto nizawadi kutoka kw mungu.

Hii ni mara ya kwanza kwa viongozi na waumini wa kanisa la Anglikana tanzania kutoa misaada kwa kituo kinachomilikiwa na kanisa la KKKT jambo ilalotafsiriwa kama kukomaa kwa upendo miongoni mwa madhehebu ya kikristo.

Mwandishi: Zawadi Paschal, Bukoba

Mhariri: Prosper Kwigize

Post a Comment

0 Comments