Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia
Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi kama ifuatavyo:
i.
Amemteua Bw. Anamringi Macha kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga. Kabla ya uteuzi Bw. Macha alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha
Mapinduzi (CCM).
ii.
Amemteua Bi. Christina Mndeme kuwa Naibu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira). Kabla ya uteuzi, Bi. Mndeme
alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
iii.
Amemteua Bw. Japahari Kubecha Mghamba kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Lushoto. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Mghamba alikuwa Katibu Tawala wa
Wilaya ya Busega.
iv.
Amemteua Bw. Mussa Kilakala kuwa Mkuu wa Wilaya ya
Pangani. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kilakala alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya
Kaliua.
v.
Amemteua Bw. Robert Masunya kuwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Kabla ya uteuzi huu Bw. Masunya alikuwa
Afisa Mwandamizi katika Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Waanawake na
Makundi Maalum.
vi.
Amemteua Bi. Mwashabani Mrope kuwa Mkurugenzi Mtendaji
wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe.
vii.
Amemteua Bw. Jacob Simon Nkwera kuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba. Kabla ya uteuzi huu, Bw. Nkwera
alikuwa Afisa Mwandamizi, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
viii.
Amemteua Bw. Sangai Mambai kuwa Katibu Tawala wa
Wilaya ya Busega.
ix.
Amemteua Bw. Raymond Mweli kuwa Katibu tawala wa
Wilaya ya Kaliua.
x.
Amemhamisha Bw. Frederick Damas Dagamiko kutoka
Halmashauri ya Manispaa ya Songea kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya Jiji la Tanga.
xi.
Amemhamisha Bw. Bashir Muhoja kutoka Halmashauri ya
Wilaya ya Iringa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya
Songea.
xii.
Amemhamisha Bw. Tito Philemon Mganwa kutoka
Halmashauri ya Mji wa Korogwe kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya
Wilaya ya Chamwino.
Uapisho wa Wakuu wa Mikoa na Naibu Katibu Mkuu
utafanyika tarehe 13 Machi, 2024 saa 04.00 asubuhi, Ikulu Dar es Salaam.
0 Comments