Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi, utenguzi na uhamisho waviongozi kama ifuatavyo:
i) Amemteua Mhe. Deogratius John Ndejembi (Mb.) kuwaWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
Kabla ya uteuzi huu Mhe. Ndejembi alikuwa NaibuWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa (TAMISEMI). Mhe. Ndejembianachukua nafasi ya Mhe. Prof. Joyce Lazaro Ndalichako ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
ii) Amemteua Bw. Paul Christian Makonda kuwa Mkuu waMkoa wa Arusha. Kabla ya uteuzi huu Bw. Makondaalikuwa Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo waChama cha Mapinduzi (CCM). Anachukua nafasi yaMhe. John Vianney Mongella ambaye atapangiwakazi nyingine.
iii) Amemteua Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuuwa Mkoa wa Mara. Kabla ya uteuzi huu KanaliMtambi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga.
iv) Amemhamisha Mhe. Said Mohamed Mtanda kutokaMkoa wa Mara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa waMwanza. Mhe. Mtanda anachukua nafasi ya Mhe. Amos Gabriel Makalla ambaye atapangiwa kazinyingine.
v) Amemteua Mhe. Zainab Athuman Katimba (Mb.) kuwaNaibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Mhe. Zainab anachukua nafasi ya Mhe. DeogratiusJohn Ndejembi (Mb.) ambaye ameteuliwa kuwaWaziri.
vi) Amemteua Mhe. Daniel Baran Sillo (Mb.) kuwa NaibuWaziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Mhe. Silloanachukua nafasi ya Mhe. Jumanne Abdallah Sagini(Mb.) ambaye amehamishwa kwenda kuwa NaibuWaziri wa Wizara ya Katiba na Sheria.
vii) Amemhamisha Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi (Mb.) kutoka Wizara ya Maji kwenda kuwaNaibu Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano naTeknolojia ya Habari.
viii) Amemhamisha Mhe. Kundo Andrea Mathew (Mb.) kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojiaya Habari kwenda kuwa Naibu Waziri wa Wizara yaMaji.
ix) Amemteua Bw. Fakii Raphael Lulandala kuwa Mkuuwa Wilaya ya Simanjiro. Kabla ya uteuzi huu Bw. Lulandala alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijanawa Chama cha Mapinduzi (UVCCM).
x) Amemteua Bw. Gilbert Kalima kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kalima alikuwaKatibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi.
xi) Amemhamisha Mhandisi Cyprian John Luhemejakutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na WenyeUlemavu) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi yaMakamu wa Rais (Muungano na Mazingira).
xii) Amemhamisha Bi. Mary Ngelela Maganga kutokaOfisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) kwenda kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu).
xiii) Amemteua Dkt. Edwin Paul Mhede kuwa NaibuKatibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi. Dkt. Mhede aliwahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala waMabasi Yaendayo Haraka (DART).
Dkt. Mhede anachukua nafasi ya Bi. Agnes KisakaMeena ambaye amehamishwa kuwa Naibu KatibuMkuu, Wizara ya Maji.
xiv) Amemteua Dkt. Suleiman Hassan Serera kuwa NaibuKatibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa naMichezo. Kabla ya uteuzi huu Dkt. Serera alikuwaMkuu wa Wilaya ya Simanjiro.
Dkt. Serera anachukua nafasi ya Bw. NicholausMkapa ambaye amehamishwa kwenda kuwa NaibuKatibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano naTeknolojia wa Habari.
xv) Amemteua Bw. Selestine Gervas Kakele kuwa Balozi. Kabla ya uteuzi huu Bw. Kakele alikuwa NaibuKatibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano naTeknolojia ya Habari.
xvi) Amemteua Balozi Dkt. Asha Rose Migiro kuwaMjumbe wa Tume ya Mipango.
Uapisho wa Waziri, Wakuu wa Mikoa, Naibu Mawaziri naNaibu Makatibu Wakuu utafanyika tarehe 04 Aprili, 2024 saa05:00 asubuhi Ikulu, Dar es Salaam.
0 Comments