BREAKING NEWS- UTEUZI - RAIS Ateua wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi



Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa Mikoa, makatibu tawala wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za miti na wilaya huku wengine wakihamishwa kutoka vituo vyao vya awali kwenda vituo vingine

Taarifa kutoka Ikulu zinaeleza kuwa, walioguswa na uhamisho huo ni pamoja na Mkuu wa mkoa wa Tabora, Singida, Iringa, na Songwe, Mkoa wa Kigoma nao umeguswa na uhamisho ambapo Katibu tawala wa mkoa huo amehamishiwa mkoa wa Katavi huku wakurugenzi wa halmashauri za Kasulu TC na Kasulu DC nao wakihamishiwa vituo vingine.

Soma hapa chini kwa kina

MABADILIKO MADOGO YA WAKUU WA MIKOA, MAKATIBU TAWALA WA

MIKOA, WAKUU WA mLAYA NA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI

Katika kuboresha utendaji kazi wa Serikali, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Wakuu wa Mikoa,

Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART). Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:

A)   Uteuzi na Uhamisho wa Wakuu wa Mikoa

Uteuzi

1.      Mhe. Lt. Col. Patrick Kenan Sawala aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara;

2.      Bw. Paul Matiko Chacha aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi ameteuliwa kuwa

Mkuu wa Mkoa wa Tabora; na

3.      Bw. Daniel Godfrey Chongolo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe.

Uhamisho

1.      Mhe. Col. Ahmed Abbas Ahmed amehamishwa kutoka Mkoa wa Mtwara kwenda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma;

2.      Mhe. Halima Omar Dendego amehamishwa kutoka Mkoa wa Iringa kwenda kuwa

Mkuu wa Mkoa wa Singida;

3.      Mhe. Peter Joseph Serukamba amehamishwa kutoka Mkoa wa Singida kwenda kuwa

Mkoa wa Iringa; na

4.      Mhe. Batilda Salha Burian amehamishwa kutoka Mkoa wa Tabora kwenda kuwa

Mkuu wa Mkoa wa Tanga.

B)   Uhamisho wa Makatibu Tawala wa Mikoa

1.      Bw. Msalika Robert Makungu amehamishwa kutoka Mkoa wa Mara kwenda kuwa

Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa;

2.      Bw. Gerald Musabila Kusaya amehamishwa kutoka Mkoa wa Rukwa kwenda kuwa

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara;

3.      Bw. Albert Gabriel Msovela amehamishwa kutoka Mkoa wa Kigoma kwenda kuwa

Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi;

4.      Bw. Hassan Abbas Rugwa amehamishwa kutoka Mkoa wa Katavi kwenda kuwa

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma;

5.      Bi. Rehema Seif Madenge amehamishwa kutoka Mkoa wa Dar es Salaam kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma;

6.      Bw. Stephen Mashauri Ndaki amehamishwa kutoka Mkoa wa Ruvuma kwenda kuwa

Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera; na

7.      Bw. Toba Alnason Nguvila amehamishwa kutoka Mkoa wa Kagera kwenda kuwa

Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam.

C)   Uteuzi na Uhamisho wa Wakuu wa Wilaya

Uteuzi

1.      Bw. Abdallah Mohamed Nyundo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilwa;

2.      Bw. Festo Kiswaga ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli;

3.      Col. Evans Alfred Mtambi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga;

4.      Bi. Alnnishi Issa Hazali ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hanang'; na

5.      Bw. Joachim Nyingo ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo.

Uhamisho

1.      Mhe. Deusdedith Josephat Katwale amehamishwa kutoka Wilaya ya Chato kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora;

2.      Mhe. Janeth Peter Mayanja amehamishwa kutoka Wilaya ya Hanang' kwenda kuwa

Chamwino;

3.      Mhe. Julius Sunday Mtatiro amehamishwa kutoka Wilaya ya Tunduru kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga;

4.      Mhe. Johari Mussa Samizi amehamishwa kutoka Wilaya ya Shinyanga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Misungwi;

5.      Mhe. Hassan Omary Bomboko amehamishwa kutoka Wilaya ya Ukerewe kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ubungo;

6.      Ivfhe. Christopher Emily Ngubiagai amehamishwa kutoka Wilaya ya Kilwa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe;

7.      Mhe. Veronica Arbogast Kessy amehamishwa kutoka Wilaya ya Iringa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbulu;

8.      Mhe. Kheri Denice James amehamishwa kutoka Wilaya ya Mbulu kwenda kuwa

Mkuu wa Wilaya ya Iringa;

9.      Mhe. Eng. Paskasi Damian Muragili amehamishwa kutoka Wilaya ya Singida kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe;

10.  Mhe. Said Juma Nkumba amehamishwa kutoka Wilaya ya Bukombe kwenda kuwa

Mkuu wa Wilaya ya Chato;

11.  Mhe. Simon Kemori Chacha amehamishwa kutoka Wilaya ya Sikonge kwenda kuwa

Mkuu wa Wilaya ya Tunduru;

12.  Mhe. Hashim Abdallah Komba amehamishwa kutoka Wilaya ya Ubungo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita;

13.  Mhe. Cornel Lucas Boniphace Magembe amehamishwa kutoka Wilaya ya Geita kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Sikonge;

14.  Mhe. Peres Boniphace Magiri amehamishwa kutoka Wilaya ya Kilolo kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyasa;

15.  Mhe. Kisare Matiku Makori amehamishwa kutoka Wilaya ya Moshi kwenda kuwa

Mkuu wa Wilaya ya Mbinga;

16.  Mhe. Aziza Ally Mangosongo amehamishwa kutoka Wilaya ya Mbinga kwenda kuwa

Mkuu wa Wilaya ya Mafia;

17.  Mhe. Zephania Stephan Sumaye amehamishwa kutoka Wilaya ya Mafia kwenda kuwa

Mkuu wa Wilaya ya Moshi;

18.  Mhe. Lt. COI. Michael Mangwela Mtenjele amehamishwa kutoka Wilaya ya Tarime kwenda kuwa Tandahimba

19.  Mhe. Col. Maulid Hassan Surumbu amehamishwa kutoka Wilaya ya Mkinga kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime;

20.  Mhe. Zainab Abdallah Issa amehamishwa kutoka Wilaya ya Pangani kwenda kuwa

Mkuu wa Wilaya ya Muheza;

21.  Mhe. Faidha Suleiman Salim amehamishwa kutoka Wilaya Itilima kwenda kuwa

Mkuu wa Wilaya ya Busega;

22.  Mhe. Anna Joram Gidarya amehamishwa kutoka Wilaya ya Busega kwenda kuwa

Mkuu wa Wilaya ya Itilima;

23.  Mhe. Gift Isaya Msuya amehamishwa kutoka Wilaya ya Chamwino kwenda kuwa

Mkuu wa Wilaya ya Bahi;

24.  Mhe. Godwin Crydon Gondwe amehamishwa kutoka Wilaya ya Bahi kwenda kuwa

Mkuu wa Wilaya ya Singida; na

25.  Mhe. Joshua Samwel Nassari amehamishwa kutoka Wilaya ya Monduli kwenda kuwa

Mkuu wa Wilaya ya Magu.

D)   Uteuzi na Uhamisho wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri

Uteuzi

1.      Dkt. Rogers Jacob Shemwelekwa ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa

Halmashauri ya Mji wa Kibaha;

2.      Bw. Masud Salum Kibetu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya

Manispaa ya Kahama;

3.      Dkt. Amon David Mkoga ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya

Wilaya ya Karagwe;

4.      Bw. George Stanley Mbilinyi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa

Halmashauri ya Wilaya ya Bunda;

5.      Bw. Murtallah Sadiki Mbillu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro;

6.      Bi. Ummy Mohammed Wayayu ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa

Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela;

7.      Dkt. Vumilia Julius Simbeye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu;

8.      Bw. Jamal Idrisa Abdul ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mlimba;

9.      Bw. Mashaka Said Mfaume ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hal-mashauri ya Wilaya ya Mufindi; na

10.  Bw. Fred Albert Millanzi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza.

Uhamisho

1.      Bw. Nassoro Bilal Shemzigwa amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido;

2.      Bw. Said Majaliwa amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Tanga kwenda kuwa

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kondoa;

3.      Bw. Paul Mamba Sweya amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Kondoa kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya;

4.      Bw. Stephen Edward Katemba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya

Sumbawanga;

5.      Bw. Semistatus Hussein Mashimba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya

Kasulu;

6.      Bw. Josephat Kashushuru Rwiza amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya

Kasulu kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga;

7.      Bw. Juma Haji Juma amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Bunda;

8.      Bw. Emmanuel John Mkongo amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Bunda kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Morogoro;

9.      Bw. Stephano Bulili Kaliwa amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo;

10.  Bw. Mohamed Ramadhan Ntandu amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya

Nsimbo kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Magu;

11.  Bi. Fidelica Gabriel Myovella amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Magu kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hal-mashauri ya Mji wa Mafinga;

12.  Bw. Ayubu Juma Kambi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Mafinga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hal-mashauri ya Wilaya ya Itigi;

13.  Bw. John Kulwa Mgalula amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Itigi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi;

14.  Bi. Faraja Paschal Msigwa amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima;

15.  Bi. Elizabeth Mathias Gumbo amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Itilima kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea;

16.  Bw. Dollar Rajab Kusenge amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Kasulu kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino;

17.  Bw. Kibamba Kiomoni Kiburwa amehamishwa kutoka Halmashuri ya Manispaa ya

Ilemela kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza;

18.  Bw. Aron Kagurumjuli amehamishwa kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo;

19.  Bw. Mshamu Ally Munde amehamishwa kutoka Halmashauri ya Mji wa Kibaha kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Nanyamba;

20.  Bw. Anderson David Msumba amehamishwa kutoka Halmashauri ya Manispaa ya

Kahama kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi;

21.  Bw. George Emmanuel Mbilinyi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya

Lindi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe;

22.  Bw. Charles Edward Fussi amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani;

23.  Bw. Isaya Mugishangwe Mbenje amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya

Pangani kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Muleba;

24.  Bi. Annastazia Tutuba Ruhamvya amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya

Same kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni; na

25.  Bw. Jimson Peter Mhagama amehamishwa kutoka Halmashauri ya Wilaya ya

Manyoni kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same.

E) Uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa UDART

1. Bw. Waziri Waziri Kindamba aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART). Bw. Kindamba anachukua nafasi ya Bw. Gilliard Wilson Ngewe ambaye atapangiwa kazi nyingine.

Uteuzi huu unaanza leo tarehe 09 Machi, 2024 na uapisho wa Wakuu wa Mikoa utapangwa baadaye.



Post a Comment

0 Comments