Rais wa Jamhuri ya Mungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa taasisi za kiserikali na
sekta binafsi kufanya jitihada za kuhakikisha wanawake wanapata nafasi na
kusikika kwenye maamuzi mbalimbali nchini.
Rais Samia amesema hayo leo kwenye mkutano wa wanawake walio katika sekta ya fedha uliofanyika ukumbi wa hoteli ya Kwanza iliyopo Kizimkazi.
Aidha, Rais Samia amesema ushiriki wa wanawake kwenye ngazi za maamuzi ni suala jumuishi na endelevu hivyo halipaswi kuchukuliwa kama la kimapinduzi au la serikali pekee.
Rais Samia amebainisha kuwa lengo ni kuhakikisha masuala yanayowahusu wanawake ambayo wafanya maamuzi wengine wanaweza wasiwe na uelewa nayo yanapata nafasi kwenye meza ya maamuzi.
Hali kadhalika, Rais Samia
amesema pamoja na kuongeza ushiriki wa wanawake kwenye ngazi za maamuzi lazima
pia kuweka nguvu kubwa katika kuwainua wanawake kiuchumi.
Kwa upande mwingine, Rais Samia amewataka wanawake kujipanga
na kufikia malengo yao kwa vitendo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na wageni
mbalimbali kabla ya kuzindua Chama cha Wanawake Sekta ya Fedha Tanzania
(TAWiFA), Kizimkazi, Zanzibar, tarehe 14 Machi, 2024.
0 Comments