Wanawake wilayani Kasulu mkoani Kigoma wameiomba selikali kupunguza bei ya gesi ili kuondoa madhila yanayowakabilii wanawake mkoani Kigoma wakati wa utafutaji wa kuni na mkaa.
Rai hiyo imetolewa na baadhi ya wananchi wa mjini Kasulu wakati wakizungumza na Buha News leo hii wakati wa kipindi cha wanawake na tabianchi.
Akizungumza katika majadiliano Bi. Leonia Kimena ambaye ni mfanyabiashara za chakula maarufu “mama lishe”, amesema wanawake wamekuwa wakikumbwa na changamoto nyingi wakati wakutafuta kuni na mkaa ikiwemo kutishiwa kubakwa na kuporwa.
Amesema kuwa wanawake wengi hasa wa kipato cha chini hutumia mda mrefu kutafuta nishati ya kupikia na kupelekea kuleta migogoro katika ndoa zao pamoja na magonjwa yatokanayo na moshi au vumbi la mkaa.
Bi. Leonia Kimena (kushoto) mama lishe Kasulu, Sara Mataro (katikati) mwanndishi wa habari na Bw. Alex Kayanda (kulia) katika picha ya pamoja baada ya kumaliza mahojiano.
Bi. Kimena amesema baadhi familia wanaume hawaamini kuwa mabadiliko ya tabianchi yanaweza
kusababisha matumizi makubwa ya mda kutokana na misitu kuharibiwa na shughuli
za binadamu na kupungua kwa miti inayotumiwa na jamii kwa ajili ya nishati ya
kupikia.
Bw. Kayanda ambaye pia ni Baba lishe ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wanaume kujenga tabia ya kuwaamini na kuwasaidia wake zaoo katika shughuli za nyumbani ikiwemo kununua gesi ili kuwaepusha na hatari zinazoweza kuwakuta wawapo katika harakati za kutafuta kuni porini
Kayanda amesisitiza kuwa, uharibifu wa mazingira unaodhihirishwa na mabadiliko ya tabianchi unasababisha Maisha kuwa magumu kwa jamii na kutoa wito kwa serikali kutoa elimu itakayosaidia wananchi kupunguza uharibifu wa mazingira sambamba na kurahisisha upatikanaji wa nishati mbadala
Utegemezi wa Matumizi ya kuni na mkaa imetajwa kua miongoni mwa
vyanzo vya uharibifu wa mazingira vinavyo pelekea mabadiliko ya tabia nchi .ambayo
huwa na athari nyingi zikiwemo na ukame au mafuliko Pamoja na joto kali.
Kigoma
ni miongoni mwa mikoa ambayo bado ina ardhii oevu na misitu asilia inayochangia
upatikanaji wa hewa safi na kupunguza hewa ukaa,, hata hivyo hivi karibuni kueripotiwa
kuwepo kwa uvamizi mkubwa wakulima na wafugani katika misitu iliyohifadhiwa.
Mwandishi: Sara Mataro
Mhariri:
Prosper Kwigize
0 Comments