MPYA: Marais Museveni na Rutto wapo Zanzibar kuteta na mama

Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Rais wa Kenya William Ruto Ikulu Ndogo Tunguu Zanzibar

Ziara hiyo maalumu ni moja ya mikakati ya kuifanya Afrika mashariki kuwa na umoja thabiti utakaowawezesha wananchi wa nchi hizo rafiki kihistoria kuishi kwa amani na kukuza uchumi utakaoivuta dunia kuithamini Afrika.

Kwenye mazungumzo yao wamezungumzia masuala ya mtangamano wa Afrika Mashariki hususan umuhimu wa kuharakisha zoezi la kukusanya maoni ya Wananchi Juu ya muundo na maeneo ya kuangaliwa katika Rasimu ya Katiba ya Fungamano la kisiasa la Afrika Mashariki  (EAC Political Confederation).  Zoezi hilo limeshafanyika katika nchi za Burundi, Uganda na Kenya na linatekelezwa na Timu ya Wataalamu inayoundwa na Wajumbe watatu kutoka kila nchi Mwanachama.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Rais William Ruto wa Kenya wakiangalia picha ya Viongozi wa Nchi mbalimbali za Afrika wakati Rais Museveni alipomkabidhi Rais Samia zawadi hiyo baada ya mazungumzo yao Ikulu ndogo Tunguu Zanzibar tarehe 14 Machi, 2024.

 


 

Post a Comment

0 Comments