Prof. Ndalichako aikuna Kamati ya Bunge, yaridhia Bajeti ya ofisi ya Waziri Mkuu

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeridhia Mpango na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Aidha, Kikao cha kamati hiyo kimefanyika leo Machi 21, 2024 bungeni jijini Dodoma kikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Fatuma Toufiq ambapo ameipongeza Wizara hiyo kwa kuandaa bajeti ambayo itawezesha utekelezaji wa majukumu sambamba na kuleta mageuzi katika sekta ya Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, Mhe. Fatuma Toufiq (kushoto) akiongoza kikao cha kamati hiyo kupokea taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya ofisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2023 hadi Februari, 2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25, kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma Machi 21, 2024. Kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Bi. Rehema Kipera.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na Menejimenti pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo Bungeni, Jijini Dodoma leo Machi 21, 2024 baada ya kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya ofisi hiyo kwa kipindi cha kuanzia mwezi Julai 2023 hadi Februari, 2024 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/25, kwa Kamati hiyo.

Katika kikao hicho Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameongozana na Naibu Waziri wa ofisi yake Mhe. Patrobas Katambi pamoja na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mhe. Mhandisi Cyprian Luhemeja kuiongoza menejimenti na Wakuu wa taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kuwasilisha bajeti hiyo.

 


Post a Comment

0 Comments