Rais Samia ana nia thabiti ya uchaguzi huru na wa Haki - Kinana

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Abdulrahmani Kinana, amewatoa hofu wanasiasa uchaguzi mkuu ujao utakuwa huru na wa haki, kwani serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano, inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, imedhamiria kuheshimu haki ya demokrasia ya vyama vingi.


Kinana ameyasema hayo leo Machi 5, 2024, jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa salamu akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndg. Samia Suluhu Hassan katika mkutano mkuu wa chama cha ACT -Wazalendo

Alisema hakuna haja wa kuwa na hofu ya uchaguzi Mkuu kwa vile serikali inayoongozwa na Rais Samia tayari imeshaweka mazingira bora yataufanya uchaguzi huo kuwa huru na haki.

"Uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao utakuwa wa huru na wa haki, wakati nazungumza hivi nina hakika wapo ambao wana mashaka na kauli hii, na hao wenye mashaka wanazo sababu, na sababu zao zinatokana na 2019 na 2020 huo ndio ukweli", alisema Kinana.
Alisema hivi sasa wanajiandaa kwenda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ambapo sasa kumefanyika mabadiliko ya sheria tatu katika Bunge lililopita.

Akizitaja sheria hizo alisema ya vyama vya siasa, Tume ya Uchaguzi na ya uchaguzi, ambayo ilitoa nafasi ya kupata maoni kutoka kwa wadau mbali mbali katika kamati za Bunge, na baadae ilitolewa maamuzi ambayo imesababisha kuwapo kwa mabadiliko makubwa sana.

“Nataka niwahakikishie serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Samia, ina dhamira ya dhati katika mwaka huu wa uchaguzi na serikali za mitaa na mwaka ujao kwenye serikali kuu kwa kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi utakuwa huru na wa haki” alisema Kinana.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Abdulrahmani Kinana, akisalimiana na kiongozi mkuu wa  Chama Cha ACT WazalendoNdg. Zitto Kabwe alipowasili Katika Mkutano Mkuu wa Chama Hicho uliofanyika Katika Ukumbi wa Mliman Dar Es Salaam


Alisema hiyo ni kutokana na kwamba kuna sheria na dhamira kwani unaweza kuwa na sheria nzuri lakini kama huna dhamira unaweza ukaikanyaga na ukafanya unavyotaka.

“Unaweza kuwa na dhamira nzuri, na sheria mbaya dhamira ikitawala mambo yatakuwa mazuri nataka ni wahakikishie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ameamua kwamba uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao utakuwa huru na wa haki, wakati nazungumza hivi nna hakika wako ambao wanamashaka na kauli hii na hao wenye mashaka wanazo sababu na sababu zao zinatokana na 2019 na 2020 huo ndio ukweli” alisema Kinana na kuamsha shangwe kutoka kwa wanachama wa chama hicho.

Alisema sheria ya uchaguzi iliopo ambayo iliwapeleka katika uchaguzi wa 2015, iliwezesha wanachama kutoka upinzani 117 kuingia Bungeni na sheria hiyo hiyo iliwawezesha karibu asilimia 40 ya Madiwani kuingia kwenye nafasi za Halmashauri na walipokuja 2020 

Msema Kweli lazima tuseme ukweli hofu ya Watanzania hofu ya wenzangu vyama vya siasa, asasi za kiraia, baadhi ya viongozi wa dini msingi wa hofu yao ni yale yaliotokea 2019 na 2020, niwahakikishie Rais Samia Suluhu Hassan, ameamua kwamba uchaguzi mwaka huu na mwaka ujao utaachwa ili wapiga kura uamuzi wao tafsiri ya uchaguzi” alisema.

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, Abdulrahmani Kinana (wa nne kushoto), akiwa na wageni wengine waalikwa akimwakilisha Mwenyekiti wa CCM Taifa Ndg. Samia Suluhu Hassan Katika Mkutano Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo  Katika Ukumbi wa Mliman Dar Es Salaam, Leo (Picha na Fahadi Siraji)

Hali hiyo alisema itafanyika katika uchaguzi wa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano kukubali kufanya marekebisho kwa namna walivyokubaliana Bungeni ni kutokana na dhamira ya viongozi wa nchi hii kutaka uchaguzi ufanyike kwa uhuru na haki.

Niliwahi kusema huko nyuma na nnarudia tena hakuna mswada uliopewa muda mrefu wa kusikilizwa na wadau kama hii miswada mitatu miswada yote hupewa nusu siku au siku nzima lakini miswada hii ilipewa siku nne, miswada hii ilikuwa ijadiliwe kwa siku moja kwa umuhimu wake umejadiliwa kwa siku nne na misawada hii imefanyiwa marekebisho mengi sana kiasi kwamba hata Rais ameridhia yeye asiteuwe Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti na badala yake apendekezewe” alisema Kinana.

Akiendelea alisema kama sheria hiyo sio nzuri kama iliyopitishwa leo iliyoweza kuwapeleka Wabunge 117 Bungeni na sasa ipo sheria bora zaidi, ni vyema wanasiasa wakaimini dhamira ya Rais na serikali yake.

Akimzungumzia Mgombea aliyejitoa katika uchaguzi wa Chama hicho Juma Duni Haji, alisema amepitia mambo mengi na mazito, mazuri na mengine yenye kuhuzunisha lakini amebaki kuwa imara na ameweka mbele maslahi ya watanzania kuliko maslahi yake binafsi.

Alisema uamuzi wake wa kujitoa katika uchaguzi huo umedhihirisha kama anajali maslahi ya taifa kuliko kujijali yeye mwenyewe binafsi.

Post a Comment

0 Comments