Ombi hilo limetolewa na wa umoja ummoja wa akina mama wakati wa maadhimisho ya siku ya wananwake duniani ambayo kimkoa yalifanyika kata ya Makere wilayani Kasulu march 8 ambapo wadau mbalimbali walihudhuria.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa mkoa wa kigoma mh Thobias Andengenye, mwakilishi wa wanawake hao Bi. Zuena Hassani ambaye ni mwanachama wa kikundi cha Malezi Chanya alisema kuwa, kusitishwa kwa mikopo hiyo imekua pigo kubwa kwa wanawake wa mkoa wa Kigoma katika kutatua changamoto za maisha zinazowakabiri.
Alisisitiza kuwa wanawake wengi wameshindwa kufanya shughuli za kijamii kutokana na kukosa mitaji hali inayo pelekea kuwa na maisha duni na kuporomoka kwa maendeleo ya kijamii.
Akijibu risala hiyo mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Kigoma Mh. Thobias Andengenye amesema changamoto hiyo ya kurejeshewa kwa mikopo inayotokana na ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri ameichukua na ameahidi kuitatua
Mh. Andengenye ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wanawake kuchangamkia fursa za kazi na kujiajili katika sekta isiyo rasmi kwa kutekeleza sshughuli mbalimbali kama vile kilimo na ufugaji.
Amesisitiza kuwa nje ya mikopo ya asilimia nne kwa kina mama, ipo mikopo itolewayo na taasisi zisizokua za kiserikali ambapo wanawake wanawezeshwa na kufundishwa namba ya kubuni na kusimamia miradi yao
Katika kusherehekea siku ya wanawake duniani, Mkuu wa mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye alitoa vyeti kwa baadhi ya vikundi vya akina mama wa mkoa wa kigoma vilivyofanya vema ili kuvipa motisha ya kufanya kazi kwa juhudi na kuepuka kuwa tegemezi katika familia.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
huazimishwa kila mwaka march 8 ambapo katika mkoa wa Kigoma yameazimishwa
katika kata ya Makere wilayani kasulu chini ya kauli mbiu “Wekeza kwa mwanamke ili kuharakisha
maendeleo kwa taifa na jamii.
Mwandishi: Sara Mataro
Mhariri: Prosper Kwigize
0 Comments