Mkuu wa mkoa wa Kigoma
Mh. Thobias Andengenye avitaka Vyuo vya ufundi kutoa mafunzo na ujuzi
utakaowasaidia wahitimu kujiajiri badala kutegemea kuomba ajira
Amesema hayo
wakati akizindua Makala maalumu iliyotengenezwa na Chuo cha maendeleo ya
wananchi (FDC) Kasulu ikionesha namna wasichana wanavyoweza kujiajiri baada ya
kupata mafunzo katika chuo hicho.
Mh. Andengenye amesema
vyuo vinavyotoa mafunzo ya ufundi havina budi kutaathimini ufundishaji wao na
kuhakikisha wanazalisha wataalumu watakaobuni na kutekeleza miradi na kuwaajiri
wenzao badala ya waomba ajira
“Rai yangu
kwenu mimi nimekuwa nikipokea simu nyingi sana kutoka kwa vijana ambao wamesoma
VETA na wengine vyuo vya maendeleo ya wananchi kama hicho cha kwenu wakitaka
niwasaidie kutafuta kazi, hivi vitu viwili vinachanganya, mimi ninaomba watu
wanaotoka FDC na VETA wasiwe wanatafuta ajira badala yake watafute kazi”
anahimiza mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye
Amesisitiza kuwa
ajira ziko chache ukilinganisha na kazi na kwamba Tanzania haijawahi kuwa na changamoto
ya kazi bali ajira ukilinganisha nan chi za Jirani ambako hata kupata kazi ni
vigumu
“Sisi tunajua
Ninyi mnazalisha wakurugenzi wanaokuja kuongeza ajira siyo kuomba ajira, kuanzia
mwanzo wakifika watambue kuwa wao ni wataalamu waajiri wataarajiwa wanaokuja
kuongeza ajira, wakimaliza vyuo wakawaajiri wengine ambao hawana ujuzi kama wao”
amesisitiza.
Amebainisha kuwa
serikali inatoa mikopo kwa vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu kutoka
katika asilimia kumi za mapato ya Halmashauri ambao hukopeshwa ili kuwajengea
uwezo katika miradi yao ili wawaajiri wengine
Mkuu wa chuo cha
maendeleo Kasulu Mwl. Fridegarda Mukyanuzi akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa
aliyetembelea bada la chuo hicho alibainisha kuwa FDC inatoa mafunzi mbalimbali
kwa vijana hususani wasichana na wanawake waliokatisha masomo ya sekondari kwa
sababu mbalimbali
Mwl. Mukyanuzi
alibainisha kuwa kupitia katika kozi zitolwazo katika chuo hicho wasichana
wameonesha mwamko wa kujifunza fani za Umeme, Uashi, uselemara, mapambo na urembo
na kwamba Makala ya video iliyoandaliwa inaonesha shuhuda mbalimbali.
Chuo cha maendeleo
ya wananchi (FDC) Kasulu kinatoa mafunzo ya ufundi stadi na teknolojia ya Habari
na mawasiliano (TEHAMA) kupitia kozi fupi na ndefu kwa kushirikiana na taasisi
ya Karibu Tanzania Association (KTO) ambao ni asasi ya Pamoja kati ya Tanzania na
Sweeden wanao saidia mabinti waliokatishwa masomo kwa sababu mbali mbali kurejea
shuleni kwa kupewa elimu maalumu.
Aidha huo cha mafunzo ya Ufundi VETA Kasulu nacho hupokea vijana na kutoa mafunzo mbalimbali ya ufundi, sayansi na teknolojia ili kuwajengea uwezo vijana kupata ujuzi mbalimbali utakaowawezesha kukuza uchumi binafsi na taifa.
Imeandikwa na: Sara
Mataro
Imehaririwa na.
Prosper Kwigize
0 Comments