Uchaguzi mdogo wa madiwani unaendelea nchini, Kimbiji wapiga kura



Kata 22 za Tanzania Bara leo zinafanya uchaguzi kuchagua madiwani katika uchaguzi mgogo unaofanyika katika kata mbalimbali nchini

Kata zinazofanya uchaguzi ni pamoja na Kimbiji (Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni), Kasingirima (Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji), Ndevelwa (Halmashauri ya Manispaa ya Tabora), Mshikamano (Halmashauri ya Manispaa ya Musoma), Msangani (Halmashauri ya Mji Kibaha), Utiri (Halmashauri ya Mji Mbinga), Fukayosi (Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo), Mlanzi (Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti) na Mbingamhalule (Halmashauri ya Wilaya ya Songea).

Kata nyingine ni Isebya (Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe), Kibata (Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa), Busegwe (Halmashauri ya Wilaya ya Butiama), Kamwene (Halmashauri ya Wilaya ya Mlimba), Chipuputa (Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu), Buzilasoga (Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema), Mhande (Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba), Kabwe (Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi), Bukundi (Halmashauri ya Wilaya ya Meatu), Mkuzi (Halmashauri ya Wilaya ya Muheza) na Boma, Mtimbwani na Mayomboni (Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga).

Mpiga Kura wa Mtaa wa Ngobanya Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam akipiga kura katika kituo cha Serikali ya Mtaa Ngobanya, kumchagua diwani wa kata yake katika uchaguzi mdogo wa udiwani unaofanyika leo tarehe 20 Machi, 2024. Wagombea Udiwani 14 wanawania nafasi hiyo. 


Mpiga Kura  wa Mtaa wa Kizito Huonjwa Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam akipiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi Kimbiji, kumchagua diwani wa Kata yake katika uchaguzi mdogo wa udiwani unaofanyika leo tarehe 20 Machi, 2024. Wagombea Udiwani 14 wanawania nafasi hiyo.
 
Karani Muongozaji Mpiga Kura katika Kituo cha Kura cha Shule ya Msingi Bohari, Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam akiwasaidia wapiga kura kuangalia majina yao kama yapo katika orodha ya wapiga kura katika kituo hicho. Wapiga Kura  wa Kimbiji leo tarehe 20 Machi, 2024 wanapiga kura kumchagua diwani wao ambapo wagombea Udiwani 14 wanawania nafasi hiyo.
 
Karani Muongozaji katika Kituo cha kupigia Kura Shule ya Msingi Golani, Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam akiwasaidia wapiga kura kuangalia majina yao kama yapo katika orodha ya wapiga kura katika kituo hicho. Wapiga Kura wa Kimbiji leo tarehe 20 Machi, 2024 wanapiga kura kumchagua diwani wao ambapo Wagombea Udiwani 14 wanawania nafasi hiyo.

Karani Muongozaji katika Kituo cha kupigia Kura Serikali ya Mtaa Mikenge, Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam akiwasaidia wapiga kura kuangalia majina yao kama yapo katika orodha ya wapiga kura katika kituo hicho. Wapiga Kura wa Kimbiji leo tarehe 20 Machi, 2024 wanapiga kura kumchagua diwani wao ambapo wagombea Udiwani 14 wanawania nafasi hiyo. 

Wakala akijaza fomu kituoni

Wasimamizi wa vituo wakionesha masanduku ya kura mbele ya mawakala wakati zoezi la kupiga kura likianza.

Wasimamizi wa vituo wakionesha masanduku ya kura mbele ya mawakala wakati zoezi la Kupiga Kura likianza.

Masanduku yakifungwa na lakiri maalum mbele ya mawakala waliopo kituoni.

 
Licha ya Mvua kubwa kunyesha lakini wapiga kura hawakusita kujitokeza kupiga Kura. 

Mpiga Kura  wa Mtaa wa Mikenge Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam akipiga kura katika kituo cha wazi cha Serikali ya Mtaa Mikenge, kumchagua diwani wa Kata yake katika uchaguzi mdogo wa udiwani unafanyika leo tarehe 20 Machi, 2024. Wagombea Udiwani 14 wanawania nafasi hiyo. 

Mpiga Kura wa Mtaa wa Bohari Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam akiwa kwa msimamizi wa Kituo cha Kupigia Kura Shule ya Msingi Bohari akijaziwa karatasi ya kura, kumchagua diwani wa Kata yake katika uchaguzi mdogo wa udiwani uliofanyika leo tarehe 20 Machi, 2024. 

Wananchi wakiwa katika Kituo cha  kura Shule ya Msingi Golani.
Mpiga Kura wa Mtaa wa Bohari Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam akipiga kura katika kituo cha wazi cha Serikali ya Mtaa Mikenge, kumchagua diwani wa Kata yake katika uchaguzi mdogo wa udiwani unafanyika leo tarehe 20 Machi, 2024. Wagombea Udiwani 14 wanawania nafasi hiyo.  Kushoto ni mtu anaeruhusiwa kisheria kumsaidia mtu mwenye ulemavu macho au asiyejua kusoma na kuandika kupiga kura.

Mpiga Kura wa Mtaa wa Bohari Kata ya Kimbiji katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Dar es Salaam akipakwa wino maalum utakaomtambulisha kuwa amesha piga kura yake.
Mpiga Kura wa Mtaa wa Golani katika Kata ya Kimbiji akiwa katika Kituturi tayari kupiga kura kumchagua Diwani wa Kata ya Kimbiji katika uchaguzi mdogo unafanyika leo tarehe 20 Machi, 2024. 

Mwandishi: Mroki Mroki
Mhariri: Prosper Kwigize

Post a Comment

0 Comments