Wakazi wa Tabata wakataa tozo mpya za Taka.

Baadhi ya wakazi wa Tabata jijini Dar es Salaam wamepinga ongezeko la tozo za uzowji wa taka wakidai kuwa hawajashirikishwa

Hayo yametokea wiki hii baada ya jamii hiyo kushuhudia matangazo yenye viwango vipya yakibandikwa katika mitaa yao

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mtambani, Brigitte Nchimbi, ameungana na wananchi wa Mtaa huo kupinga ongezeko la ada ya uzoaji taka kwenye makazi ya kawaida, kutoka Sh 2,500 hadi Sh 5,000 kwa kaya.


Taarifa za ongezeko hilo  zinasambazwa na Mtumishi wa Kampuni ya BP Urasa, Rebeca Shaban, kupitia andiko lenye Nembo ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ya Halmashauri ya Ilala, lenye muhuri wa Afisa Mtendaji wa Kata ya Tabata na saini ya Afisa Afya wa Kata hiyo.

“Hili andiko silitambui, ni feki, tunalipa Sh 2,500  hakuna kikao kilichoamua tulipe Sh 3,000 au Sh 5,000, lipeni 2,5000 na wawape risiti,” Nchimbi akasema.

Afisa Mtendaji wa Kata hiyo, George Lugongo hakukiri wala kukana andiko hilo, akashauri sheria ndogo zirejewe na kwamba, anaandaa mkutano wa hadhara ambao pamoja na mengine, suala hilo litajadiliwa. 

Kwa mujibu wa Sheria ndogo za (Afya na Usimamizi wa Mazingira) za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala za Mwaka 2019, Jedwali la Kwanza lililotungwa chini ya kifungu cha 5(1) inaelekeza;

Na 2: Nyumba za chini (kwa kaya) kipato cha juu kwa mwezi ni Sh 8,000, kipato cha kati Sh 3,500 na kipato cha chini ni Sh 2,500.

Endapo mgomo huo wa viwango vya tozo hautatatuliwa ipo hatari ya kuzagaa kwa taka mitaani na kuhatarisha afya ja jamii.

Mwandishi. Editha Majura
Mhariri: Prosper Kwigize

Post a Comment

0 Comments