Wanawake wa mashirika ya UN waadhimisha siku yao kivingine


Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani 2024, Wanawake wafanyakazi wa mashirika yanayohudumia Wakimbizi mkoani Kigoma wametoa msaada wa pes ana vitu mbalimbali kwa Watoto wenye mahitaji maalumu katika kituo cha shule ya msingi Kaganga mazoezi ili kuonesha upendo wa mama.

Wanawake hao kutoka Shirika la Umoja wa mataifa linalohudumia wakimbizi duniani UNHCR kwa kushirikiana na wengine mashirika mengine ya Umoja wa mataifa na mashirika wadau wa UN wametoa taulo kwa ajili ya afya za wasichana, sabuni, dawa za meno na miswaki, vinywaji na pesa kwa ajili ya kuunganisha shule na mitandao ya mawasiliano ya kidigitali ikiwemo runinga.

Akitoa maelezo kuhusu azimio la wananwake hao kuungana kuwasaidia Watoto hao ambao wengi wao ni wenye ulemavu wa viungu, Ngozi, macho na masikio, Afisa habari wa UNHCR Ofisi ndogo za Kasulu Bi. Maimuna Mtengela amebainisha kuwa kuwasaidia Watoto ndio ishara halisi ya mwanamke kuijali, kuilinda na kuiendeleza jamii

Bi. Mtengela ameeleza kuwa Mpango huo ambao umeratibiwa na UNHCR unahusisha wanawake wanaofanya kazi katika mashirka hayo keonesha upendo wa mama kwa watu wenye mahitaji maalumu hususani Watoto

Amesisitiza kuwa baada ya kuwasisliana na mamlaka za serikali waliarifiwa kuwa Watoto wanaoishi, kusoma na kutunzwa katika kituo maalumu cha watu wenye ulemavu cha Kabanga wanakabiliwa na changamoto nyingi za kijamii ikiwemo kukosa Maisha ya malezi ya wazazi hasa kwa wenye ulemavu wa ngovi waliokimbia mauaji dhidi yao mwaka 2008-2015 na kulazimika kuishi katika kituo hicho.

“sisi wanawake tunaohudumia wakimbizi katika kambi za Nyarugusu na Nduta mkoani Kigoma tumeamua kuungana Pamoja kusherehekea siku ya wanawake duniani kitofauti, tumeamua kutoa huduma kwa Watoto hawa wenye mahitaji maalum ili kuonesha upendo kwao”

 

Maimuna Mtengela amesisitiza kuwa Mwanamke ni mama na haijalishi kuwa mtoto unayemhudumia ni wako au wa jamii nyingine hivyo kila mwanamke anatakiwa kusherehekea siku hii kwa kutoa misaada kwa Watoto ambao kwa namna moja ama nyingine wazazi wao wanashinda kutimiza mahitaji ya Watoto wao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo umasikini

Kwa upande wake afisa utawala na fesha wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM mjini Kasulu Bi. Shakila Ngilangwa amebainisha kuwa IOM imeona fahari kushiriki maadhimisho ya siku ya wananwake kwa kuungana na wanawake wote wa mashirika ya umoja wa mataifa kutoa msaada kwa watoto wenye uhitaji maalumu.

Wanawake hao kutoka Shirika la Umoja wa mataifa linalohudumia wakimbizi duniani UNHCR kwa kushirikiana na mashirika mengine ya Umoja wa mataifa na wadau wa UN wametoa taulo kwa ajili ya afya za wasichana, kama sehemu ya kuonesha thamani na wajibu wa Mwanamke katika jamii pic.twitter.com/84SJYCV8PU

— BUHA FM RADIO (@buhafm) March 8, 2024 Bi. Ngilangwa amesisitiza kuwa IOM inatambua uwepo wa watoto wenye mahitaji maalumu hususani wenye ulemavu wa ngozi ambao baada ya kufikishwa katika kituo cha usalama cha kabanga wazazi na ndugu wamewatelekeza bila kuja kuwaona jambo ambayo linawanyima haki mbalimbali za kijamii.

"Sisi kwa Mama tunatambua kuwa watoto wanahitaji malezi ya wazazi lakini hapa wapo watoto wenye ulemavu ambao kwa sababu ya ulemavu wao wametekelezwa hapa na jamii zao, hivyo siku ya wanawake duniani kwetu tumeadhimisha kwa kuwajali na kuwapa faraja" Amesisitiza Bi. Ngilangwa

Bi. Sakila Ngilangwa ambaye pia ni mwenyekiti wa wanawake wanaounda umoja wa watumishi wa kike katika mashirika ya Umoja wa Mataifa katika kambi za wakimbizi za Nyarigusu na Nduta, ametoa wito kwa wadau mbalimbali kuwatazama watoto wa shule ya msingingi Kabanga mazoezi kwa jicho maalum ili kuhakikisha wanapata mahitaji na malezi sahihi kwa ajili ya kuwa na kizazi na taifa bora lenye watoto waliopata haki za kijamii kwa usawa bila ubaguzi.

Naye mkuu wa shirika la huduma za kanisa ulimwengunei (world Church Service -WCS) Bi. Grace Waiharo yeye ameshukuru kuwa wanawake kutoka katika jamii yao wamekubali kuungana pamoja kuonesha umeme wao kwakuwa mwanamke ni Upendo na kusisitiza kuwa kila mwanamke anao wajibu wa kujali watoto hususani wenye mahitaji maalum.

Mkuu wa kitendo cha elimu maalum katika shule ya Msingi Kabanga mazoezi Mwalimu Kasmil Masolwa pamoja na kuwashukuru wanawake hao, amekiri kuwa shule yao pamoja na kituo cha watoto wenye ulemavu wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazohitaji ushirikiano wa pamoja wa wadau mbalimbali pamoja na serikali.

"Hapa tunatoa elimu jumuishi kwa watoto wote na matokeo yanaonesha kuwa watoto wenye ulemavu wanafanya vizuri zaidi katika mitihani ulikinganisha na wanafunzi wasio na mahitaji maalimu" anasisitiza Mwalimu Masolwa

Shule ya Msingi Kabanga Kasulu ina zaidi ya wanafunzi 800 ambapo kati yao wanafunzi 150 ni wenye mahitaji maalum wanaohitaji uangalizi maalumu wakiwemo wenye ulemavu wa viungo, macho, masikio, akili na ualbino.

Imeandikwa na: Prosper Kwigize

Imehaririwa na: Adela Madyane

 


Post a Comment

0 Comments