Anuani za makazi nchini zaboreshwa wananchi waonywa

Wizara ya habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imeanza kufanya maboresho ya zoezo la anuani za makazi katika manispaa ya Kigoma Ujiji kwa kusasisha taarifa na miundombinu iliyofanyika kwa kipindi kilichopita cha mwaka 2022 sambamba na kuhuisha na kukusanya taarifa mpya

Akitoa taarifa hiyo Mtaalamu wa Mfumo wa Anwani za Makazi kutoka Wizara hiyo Charles Semzaba amesema zoezi hilo linafanyika katika halmashauri 13 kote nchini na litafanyika kwa siku 14, siku mbili za mafunzo kwa watendaji wa mitaa na kata watakao shiriki katika zoezi hilo na siku 12 za ukusanyaji wa taarifa. 

Semzaba amesema awali mpango huo ulikuwa kwaajili ya uwekaji wa anwani za makazi (namba ya jengo, au kiwanja), majina ya barabara au kitongoji na postikodi ila sasa unakwenda mbali kizaidi na kuwezesha pia utambulisho wa watu, usajili wa biashara, kufanyika kwa biashara mtandaoni ambapo wafanyabiashara na wanunuzi watakuwa na uwezo wa kununua na kumfikishia mteja bidhaa, upatikanaji wa huduma za dharura kama vile polisi na huduma za zima moto.

“Maboresho ya taarifa hizi yatafanya wananchi waweze kujaza fomu na kupata barua za utambulisho kwa kutumia simu za mkononi badala ya kwenda kuomba kwa viongozi wa mtaa,na pia tumeandaa sheria ya anuani ya makazi, kila mwananchi awe na anuani ya makazi.” amesema Gombo

Akizungumza mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji Mwantum Mgonja amewaonya wananchi wanaofanya uharibifu wa vyuma vinavyoonesha mitaa na miundombinu mingine ya anwani za makazi na kuuza kama vyuma chakavu na kuwa yeyote atakayebainika atachukuliwa hatua za kisheria kwakuwa ni uhalifu.

Wataalam wa anwani za makazi kutoka wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia ya habari wakiwa katika picha ya pamoja na mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji, Mwantum Mgonja (katikati) baada ya kutoa mrejesho wa namna zoezi linavyoendelea ndani ya manispaa hiyo 

Kwa upande wa kaimu katibu tawala mkoa wa Kigoma Ntime Mwalyambi ameomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha na zinazohitajika kwani zitasaidia kuondoa mapungufu yaliyobainika kipindi cha mwaka 2022 na kupata anuani za makazi zilizo sahihi kwakuwa toka kipindi hicho mambo mengi yamebadilika na Watu wengine wamehama na wengine kuishi kiholela bila kutambulika.

Akizungumza Joyce Meta mwananchi kutoka manispaa ya Kigoma Ujiji amesema zoezi hili litasaidia namba za nyumba kuelekweka vizuri kwani kulikuwa na mkanganyiko wa namba za nyumba na mitaa

Mwandishi: Adela Madyane

Mhariri: Prosper Kwigize


Post a Comment

0 Comments