Zaidi ya milioni 12 zatolewa kama hamasa kwa walimu Kigoma.



Halmashauri ya wilaya ya Kigoma imetoa takribani milioni 12,000,000 kama motisha kwa walimu, shule na kata zilizofanya vizuri katika mtihani ya kuhitimu darasa la saba na mtihani wa kujipima wa darasa la nne kwa mwaka 2023.

Akitoa motisha hiyo wakati wa kikao cha tathimini ya matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi na upimaji wa kitaifa wa darasa la nne kwa mwaka 2023 kaimu mkurugenzi ambaye pia ni afisa elimu ya msingi wa halmsahuri hiyo Kassim Mtili amesema motisha hizo zimetolewa kwa lengo la kuhimiza ufaulu, na kuleta ushindani katika sekta ya elimu.


 “Tunafurahi kuona mwaka huu halmshauri yetu imeshika nafasi ya tatu kati ya nane zilizopo mkoani humu, nawaomba sana tufanye kazi kwa bidii ili tuweze kushika nafasi ya kwanza kimkoa kwa mwaka 2024 kwani uwezo tunao na nia ya kufanya vizuri tunayo” Amesema Mtili. 


Amefafanua kuwa halmashauri hiyo ilifanikiwa kuongeza ufaulu kwa asilimia 6.79 kutoa asilimia 80 mwaka 2022 ambapo ilishika nafasi ya nne kimkoa hadi kufikia asilimia 86.79 mwaka 2023 na kuifanya kushika nafasi ya tatu, huku kwa mwaka 2021 halmashauri hiyo ikishika nafasi ya tatu pia.


Edo Madyane, ( mwenye mic) afisa elimu taaluma shule za msingi, halmashauri ya wilaya ya Kigoma akiongoza zoezi la utoaji wa tuzo na zawadi kwa washindi.
l  
Akitoa ufafanuziwa motisha hizo, afisa elimu taaluma, Edo Madyane, amesema zimegawiwa katika makundi matatu ambapo kundi la kwanza ni kwa shule zenye watahiniwa kuanzia mmoja mpaka 40, kundi la pili lenye watahiniwa kuanzia 41-99, na kundi la tatu lenye watahiniwa 100-160 


Amesema shule zilizoibuka washindi kwa kushika nafasi ya kwanza kutoka katika makundi hayo ni shule ya msingi Kisozi,kundi la kwanza, shule ya msingi Kiganza na Mkigo kundi la pili na shule ya msingi Mgogo iliyopo kata ya Kalinzi katika kundi la tatu. 


Kwa upande wake Katibu wa tawala wa halmshauri ya wilaya ya Kigoma Mgwanwa Nzota ambaye alikuwa mgeni rasmi katika kikao hicho, ametoa ahadi kuwa endapo halmashauri ya wilaya ya Kigoma itaweza kushika nafasi ya kwanza kimkoa ofisi yake itatoa zawadi ya shilingi miloni tano, na kwa shule zitakofanya vizuri atatoa zawadi ya milioni moja. 






















Katibu wa tawala wa halmshauri ya wilaya ya Kigoma Mgwanwa Nzota akiongea na washiriki wa kikao cha tathimini kilichofanyika katika sekondari ya Mwandiga  

Akiongea mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kiganza ambaye shule yake imepokea tuzo 6, Gerlad Kizeba amesema wataendelea kufanyia kazi mikakati iliyotolewa na halmashauri hiyo ili kuhakikisha wanafanya vizuri zaidi kwa kushirikiana na wazazi, walimu, wanafunzi na wadau wengine wa elimu


Miongoni mwa mikakati iliyowekwa na halmashauri hiyo ili iweze kushika nafasi ya kwanza kimkoa ni pamoja na kufanya usajili yakinifu kwa kuzingatia mahudhurio, kukamilisha mada za ufundishaji kwa darasa la saba na la nne ifikapo mwezi Juni mwaka huu, kufanya mtihani wa majaribio kila mwezi, kuweka kambi ya masomo na kufanya mtihani wa ujirani mwema.


Imeandikwa na: Mwandishi wetu

Imehaririwa na: Prosper Kwigize

Post a Comment

0 Comments