Makala amrithi Makonda, Hapi, Mongela na Joketi waula

Siku chache baada ya Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu hassan kupangua safu ya viongozi mbalimbali katika serikali yake, huku akimteua Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Chama cha mapinduzi kimeziba nafasi zilizoachwa wazi na viongozi wake walioteuliwa ndani ya serikali.

Mwenyekiti wa CCM Dr. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamatii Kuu ya halmashaurii Kuu ya Chama Cha Mapinduzi mapema leo Jijini Dar es salaam

Ifuatayo ni taarifa yenye orodha ya walioteuliwa kutoka ndani ya Chama Cha Mapinduzi iliyotolewa baada ya kumalizika kwa Kikao maalumu cha kamati kuu ya CCM kilichofanyika Jijini Dar es Salaam mapema leo



Kutoka Kushoto ni Ali Hapi aliyeteuliwa kuwa Katibu mkuu wa Jumuiya ya wazazi, Amosi Makala katibu wa itikadi, uenezii na mafunzo na John Mongera naibu katibu mkuu Bara.

Aidha katika kikao hicho, Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imezipongeza Serikali zake zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, chini ya Rais Dkt Hussen Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kwa kazi kubwa na nzuri ya kuendelea kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020 – 2025.



Post a Comment

0 Comments