Askofu Mlola atoa wito kwa jamii kuzingatia maadili ya familia

Waamini wa Kanisa katoliki nchini wametakiwa kufunga na kuombea miito mitakatifu katika kanisa hasa miito ya mapadre na watawa ili kufanyika kuwa wachungaji wema wa kiroho na kimwili

Rai hiyo imetolewa na  Mhasham Askofu Josephu Romani Mlola wa jimbo la Kigoma April 21 wakati wa misa takatifu ya dominika ya 4 iliyo azimishwa katika parokia ya teule ya Mwilamvya Kasulu Jimbo la Kigoma ikiwa ni  wiki ya kuombea miito mitakatifu

Amefafanua  kuwa kuna umuhimu mkubwa pia wa kuombea miito ya ndoa takatifu kwani ndio  muito pekee unao leta  matokeo ya miito mikubwa ya upadre na utawa hivyo ili kupata Baraka katika maisha ya kiroho na kimwili.

Amesema  wazazi wanayo nafasi kubwa ya kuilea miito hiyo katika malezi ya Watoto kwa maadili ili kutengeneza miito miingine ya kiroho hususani wito au sakrament ya upadre na utawa

Baadhi ya Watawa wanafunzi wakishiriki Misa takatifu ya siku 60 kuombea miito ya Upadre na Utawa katika Kanisa Katoliki jimbo la Kigoma

Askofu Mlola amehimiza wazazi na jamii kutoacha jukumu la mazlezi ya Watoto kwa wasichana wa kazi (watumishi wa nyumbani) fuatilia nyendo za watoto wao na sio kuwaachia na kuwaamini wadada wa kazi bali kulinda familia na kuwa mchungaji bora katika familia.

Wakati huo huo Askofu Mlola ametumia Misa hiyo kutoa wito kwa watanzania wote kuzingatia amani wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu Pamoja na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa kuchagua viongozi wenye maadili na kuonya wanaoanza kuleta chokochoko kwa kutoa kauli zinazochochea uvunjifu wa amani

Mwandishi: Sara Mataro

  

Post a Comment

0 Comments