Breaking News: BM uso kwa uso na ‘Landcruiser’ Morogoro

Basi moja la kampuni ya BM iliyokuwa ikifanya safari zake kutoka mjini Morogoro kwenda Dodoma limepata ajali mbaya baada ya kugongana uso kwa uso na gari dogo aina ya Landcruiser

Kwa mujibu wa abiria mmoja aliyekuwa akisafiri na basi la kampuni hiyo, ajali hiyo imetokea katika wilaya ya mvumero likielekea wilayani Gairo

Abiria huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe ameiambia Buha news kwamba gari dogo aina ya Landcruiser ambalo namba zake hazikufahamika haraka liligongana na basi uso kwa uso na wakati magari hayo yaliposhindwa kupishana

Inaelezwa kuwa ajali hiyo imetokana na uzembe wa mmoja kati ya madereva wa magari hayo aliyekuwa amejaribu kulipita gari lingine lililokuwa mbele yake. “Overtaking” bila kuchukua tahadhari

Buha news inawasiliana na mamlaka za jeshi la polsi mkoani morogoro ili kuapa taarifa za kina kuhusu ajali hiyo

Post a Comment

0 Comments