Byabato ajitolea kuwalipia bima wapiga kura wake Bukoba

Watu 140 wasiojiweza katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wanatarajia kupata Bima ya afya ya Jamii iliyoboreshwa ili kuwasaidia kupata huduma za afya kwa urahisi kwenye vituo vya serikali watakapokuwa na uhitaji wa huduma hiyo.

Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Stephen Byabato amesema hayo wakati akitoa Bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa kwa wananchi 18 wa kisiwa cha Musira kilichopo kata ya Miembeni ambapo mbunge huyo ameungana na wadau mbalimbali pamoja na  wanagroup la Whatsapp la Bukoba mjini mpya kutembelea na kuzungumza na wananchi wa  kisiwa cha Musira .

Mhe Byabato amesema kuwa wananchi waliopata Bima hizo kuanzia leo watakuwa wanatibiwa bure kwenye vituo vya afya vya serikali watakapoenda kupata matibabu.

Aidha Mh. Byabato ametangaza kuwalipia bima ya afya wananchi kumi kutoka kila kata ndani ya jimbo hilo ili kuwapunguzia madhila ya kukosa bima na kutibiwa kwa gharama kubwa

Amesema kuwa Bima hizo tayari zimeshalipiwa hivyo kwa ambao wameshapata wakati watakapopata changamoto ya afya waende wakatibiwe

Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini Adv Stephen Byabato akitoa Bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa kwa baadhi ya wananchi wa kisiwa cha Musira

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wa kisiwa cha Musira waliopata Bima hizo wamemshukuru mbunge kwa kuwapa msaada huo na kukiri kuwa bima hiyo ni mkombozi kwao

Akiongea kwa niaba ya wengine moja wa wanufaika wa bima hizo amesema kuwa walikuwa wanapata changamoto ya kupata huduma za afya kwa wakati kwani wakati mwingine wanakuwa hawana pesa  hivyo Bima hizo zitawasaidi sana.

Naye Bi. Juleth Richard, akisoma risala iliyoandaliwa na Mwenyekiti wa mtaa wa Musira, amesema kuwa katika mtaa huo yapo mambo mengi ambayo yamefanyika ikiwa ni pamoja na ujenzi wa choo, Boti ya Mv Byabato na majiko ya gesi kwa mama na Baba lishe.

Mwandishi: Mariam Kagenda

Mhariri: Prosper Kwigize

Post a Comment

0 Comments