Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga ametoa wito kwa wananchi na Wabunge nchini kutembelea Maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma ili kufahamu masuala mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali chini ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Naibu
Waziri Kapinga ametoa wito huo tarehe 15 Aprili, 2024 baada ya kutembelea mabanda ya Maonesho hayo
na kujionea jinsi Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Wadau wake walivyojipanga
tayari kwa kuhudumia Wabunge na Wananchi watakaotembelea maonesho husika.
“
Nawakaribisha Wananchi na Wabunge kwenye Wiki hii muhimu sana ya Nishati,
ambapo tunaonesha kazi mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Nishati pamoja na
Taasisi zake, tunatatua kero mbalimbali zinazowasilishwa na pia Wabunge na
Wananchi watajionea utekelezaji wa miradi katika wilaya zote, majimbo yote na
mikoa yote Tanzania.” Amesema Mhe.
Kapinga
Ameongeza
kuwa, katika Maonesho hayo Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Nishati
pamoja na kampuni zake tanzu zimeshiriki.
Mhe.
Kapinga amesema kuwa, katika miaka mitatu ya uongozi wa Rais, Dkt. Samia Suluhu
Hassan kazi kubwa imefanyika katika Sekta ya Nishati akitolea mfano utekelezaji
wa miradi mbalimbali ukiwemo wa Julius Nyerere (JNHPP) ambao umeshaanza
kuzalisha umeme, miradi ya usambazaji umeme mijini, vijijini na vitongojini, nishati
safi ya kupikia pamoja na sekta ndogo ya Mafuta na Gesi Asilia.
Maonesho
ya Wiki ya Nishati yaliyoanza leo yatahitimishwa tarehe 19 Aprili 2024 ambapo
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko atayafungua rasmi
tarehe 16 Aprili 2024.
0 Comments