Wakulima wadogo wadogo wa kilimo cha umwagiliaji katika bonde la mto Bogwe mjini Kasulu mkoani Kigoma wametakiwa kufata kanuni za kilimo bora ili kuzuia uchafuzi na uhalibifdu wa vyanzo vya maji unaoweza kusababisha ukame.
Hayo yamesemwa na Afisa wa mamlaka ya maji mjini Kasulu
Bw. John Mikidadi wakati wa mahojiano na Buha News ofisini kwake kuhusu uchafuzi
wa mito unao jitokeza katika nyanzo vya maji.
Amesema baadhi ya wakulima wanafanya shughuli za
kilimo kando kando ya vyanzo vya maji hali inayo pelekea uhalibifu wa mazingira
na kusababisha maji kutoka katika mabomba yakiwa machafu.
Ameeleza kuwa kilimo kando kando ya mto athari yake ni
kupungua kwa chanzo cha maji na kusababisha madawa ya kilimo kuingia mitoni na
kuhatarisha usalama wa watumiaji wengine wa maji
Bw. Mikidadi ametumia fursa hiyo kutoa rai kwa wakulima katika maeneo ya mito na vyanzo vya maji kufuata kanuni na ushauri unao tolewa na maafisa wa kilimo na kuacha umbali wa mita 60 kutoka katika mto na kutumia vifaa vya kisasa ili kuepusha uchafuzi unajiotokeza
Kwa upande wake mmoja wa wakulima wa maeneo ya hayo Bw.
Amos Ndikulije amekiri kuwepo na uharibifu sambamba na ukiukwaji wa sheria za
mazingira na ameiomba serikali kuongeza maafisa kilimo ili kutoa elimu ya
kutosha juu ya kilimo bora.
Amesema wakulima wengi wamekuwa wakichafua vyanzo vya
maji na hata kusogeza mashamba yao karibu na mto pasipo kujua madhara yanayo
weza kujitokeza
Bw. Yese Ndiliwe ambaye ni mkulima mkongwe katika
bonge la mto Bogwe amesema wakulima hufata vyanzo vya maji ili kurahisisha
shughuli za umwagiliaji
Ameongeza kuwa wakulima wengi wanashindwa kununua
pambu za kisasa kwa ajili ya umwagiliaji kutokana na kipato duni
Akijibu malalamiko hayo afisa kilimo wa kata ya
Mwilavya Bi. Evita Rupeche amekiri kuwepo kwa changamoto ya uharibifu wa vyanzo
vya maji vitokanavyo na wakulima kunakotokana
na wakulima kukaidi maelekezo ya serikali
Amebainisha kuwa ofisi yake imekuwa ikitoa elimu kwa
njia mbalimbali ikiwemo kusambaza machapisho yanayoelekeza kuhusu kilimo bora
na endelevu
Uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji ni moja ya
sababu za mabadiliko ya tabia nchi
Mji wa Kasulu jina lake hupambwa na mto Kasulu ambao umebaki historia kufuatia kukauka kwa chanzo chake huku Mto Bogwe uliokuwa mkubwa na watu wakivuka kwa mitumbwi miaka ya 1980 uko katika hatari ya kutoweka.
Mwandishi: Sara Mataro
Mhariri: Prosper Kwigize
0 Comments