Wenyeviti wa mashina wa Chama Chama Mapinduzi wilayani
Kasulu mkoani Kigoma wamemshukuru Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini Profesa Joyce
Ndalichako kwa kutambua umhimu na mchango wa viongozi wa mashina kwa
kuwakutanisha pamoja katika mafunzo ya kuwawezesha kujua wajibu na nafasi zao
katika chama.
Shukurani hizo zimetolewa na mabalozi zaidi ya 400 mwishoni
mwa juma lililopita baada ya kupata mafunzo ya kuwajengea uwezo kuelekea
uchaguzi mkuu wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika mwaka huu
Mwamini Shem Kazara ni mwenyekiti wa shina namba 5
kata ya Murubona ni mmoja wa amesema mbali na kuwa na changamoto nyingi katika
mashina wamefuraishwa na kitendo cha mbunge kugharimia mafunzo hayo
Aidha Mwamini amekipongeza Chama Cha mapinduzi kwa
kuahidi kuanza kuwalipa posho viongozi wa mashina maarufu kama Mabalozi
kutokana na fedha zalipo ya ada ya mwanachama.
Amefafanua kuwa fedha hizo zitsaidia kufanya
mabadiliko makubwa katika uongozi wa mashina kama vile kununua mahitaji mbalimbali.
Kwa upande wake Katibu Itikadi siasa na Uenezi wa CCM
kata ya Murusi ndg. Adriani Ndorere amesema mkutano huu umewapa chachu na
motisha wenyekiti wa shina ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa kujitolea na
kukisaidia chama kupata ushindi
“Mabalozi walikuwa hawalipwi chochote walifanya kazi
kama wakereketwa wa chama na sasa Raisi Samia Suruhu Hassani ametambua mchango
wao” aliongeza Ndg Ndorere
Awali, Katibu wa CCM mkoa wa Kigoma ndugu Mobutu
Malima alitangaza kuwa Chama makao makuu kimenunua pikipiki kwa ajili ya
watendaji wake ngazi ya kata na kwamba hivi karibuni zitagawiwa ili kuwawezesha
viongozi hao kufanya kazi kwa weledi.
Bw. Malima alibainisha kuwa viongozi watakaonufaika na
mpango huo ni makatibu wa jumuiya zote Pamoja na makatibu kata wa Chama.
“Mjiandae kupokea pikipiki na mkazitumie kwa shughuli
za chama na siyo kufanya biashara ya bodaboda, na pia nawahimiza mkapate
mafunzo ya udreva katika taasisi za mafunzo ili kupata ujuzi na mhakikisha
mnapata leseni za kuendesha vyombo vya moto” Alisisitiza Malima.
Hii ni mara ya kwanza kwa mabalozi wa nyumba kumi ngazi
ya jimbo kukutanishwa na kupewa mafunzo ya wajibu wao kwa mujibu wa katiba ya
CCM katika wilaya ya Kasulu na mkoa wa Kigoma.
Mwandishi: Sara Mataro
Mhariri: Prosper Kwigize
0 Comments